MGOMBEA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI BAGAMOYO.
Ben Komba,Pwani-Tanzania/9/28/2015 10:59 AM Mgombea wa udiwani katika Kata ya Vigwaza wilaya ya Bagamoyo,Jimbo la uchaguzi Chalinze amewataka wananchi wamuunge mkono katika uchaguzi mkuu ujao kwa kumpigia kura ya ndio ili aweze kuwasaidia katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili. Mgombea huyo, BW.SADALAH CHACHA amewahakikishia wapiga kura kuwa watakapomchagua hawatajutia kura yao na hivyo amewasihi wamkopeshe kura zao ili aweze kuwalipa maendeleo. BW.CHACHA amefafanua kuwa kwa muda mrefu wananchi wa Ruvu darajani wamekuwa kama yatima na kila mwenye nguvu kuonyesha uwezo wake katika kijiji hicho na kutolea mfano wa uvamizi wa ardhi unaofanywa na wageni ili hali wenyeji wakiwa hawana ardhi ya makazi na kilimo. Amepingana na dhana ambayo serikali ya CCM inatumia ya kugawa maeneo kwa watu wanaovaa joho la uwekezaji ikiwa wanajua sio wawekezaji na wanapofika vijijini wanawalaghai wananchi kwa ahadi hewa ambazo mara nyingi hazitekel;ezwi ikiwa kama nitawajengea shu...