WANAKIJIJI WAANDAMANA BAGAMOYO
Ben Komba/Pwani-Tanzania Wananchi wa Kijiji cha Kinzagu kata ya Lugoba Tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwania wameandamana kudai utekelezaji wa makubaliano kati ya kijiji na mwekezaji. Wananchi hao waliokuwa wakiimba nyimbo za kudai haki zao kufuatia kuchoshwa na ahadi ya mwekezaji katika madini ya kokoto kijijini hapo kutototekeleza ahadi walizokubaliana wakati walipofika kuomb ardhi kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya kokoto kwa matumizi ya ujenzi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kiji hicho BW. WILLIAM MAKUMU akizungumza kwa niaba ya wakazi amesema kuwa wanaungana na wanakijiji hao kutokana na Kampuni STRABAG kuchukua ardhi kwa makubaliano wa ujenzi wa zahanati lakini baada ya kuchelewa kufanya hivyo moja ya makampuni yanayoenbdesha shughuli za uchimbaji ikajenga hivyo wakaingia makubaliano mengine ya kuwapatia umeme na kununua trekta. MAKUMU amebainisha kuwa Mkandarasi huyo kampuni ya STRABAG imekuwa ikizunguka katika utekelez...