WALAMIKIA MALIPO KIDUCHU HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/7/28/2014 6:16:35 PM Watumishi wa kitengo cha mazingira halmashauri ya mji wa Kibaha wameendelea kulazimika kufanya kazi kwa kima cha mshahara wanacholalamikia ambacho wao hawakubaliani nao. Mwandishi wa habari hizi amewashuhudia watumishi hao wakifanya kazi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya wajibu wao kuhakikisha kuwa nji wa Kibaha unakuwa safi muda wote sambamba na uwepo wa gari la kisasa la taka. Nimebahatika kuongea na watumishi hao wa mazingira ambao walikuwa na mambo kadhaa ya kuelezea, Mmoja wa BW.KASSIM MALIVI amesema wao wanalipwa shilingi 125,000/- kiwango ambacho hakitoshelezi mahitaji na kulinganisha na uzito wa kazi wanayofanya. BW.MALIVI ameongeza wamepeleka malalamiko yao sehemu mbalimbali wakitaka kuboreshewa maslahi yao, Hatua ambyo iliwafikisha hadi ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kibaha BI.HALIMA KIHEMBA ambaye aliaahidi kulishughulikia suala hilo kwa karibu. Naye mtumishi mwingine BW.JUMANNE KADALA amesema kuwa yeye ana...