TFF WAPYA WAPONGEZWA
Thursday, October 31, 2013/Ben Komba/Pwani-Tanzania/17:28:06 Mdau wa soka mkoa wa Pwani ambaye pia ni kiongozi wa vilabu amewapongeza wajumbe wa kamati ya utendaji na Rais wapya waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka Tanzania uliofanyika hivi karibuni. Akiongea na mwandishi wa habari hizi mdau mkubwa wa soka katika Mkoa wa Pwani, BW. MRISHO SWAGALA amewapongeza viongozi wapya waliobahatika kuchaguliwa katika kinyang’anyiro hicho. BW.SWAGALA amefafanua kuwa wanachotakiwa kufanya uongozi mpya ni kutumia fursa hiyo adimu kunyanyua kiwango cha mchezo wa soka nchini ambao umekuwa ukilegalega siku hadi siku kwa sababu ya kukosekana viongozi makini. Aidha ameelezea Jinsi anavyomjua Rais wa sasa wa TFF, JAMAL MALINZI kama ni mchapakazi wa ukweli na amemshuhudia mara kadhaa akitumia uwezo wake wa hali na mali kusaidia mchezo huo hususan katika Mkoa wa Pwani. END.