Posts

Showing posts from August, 2013

MWENGE UHURU

MWENGE WA UHURU Ben Komba/Pwani-Tanzania/10:55/ 30-08-2013. Mwenge wa uhuru umemaliza mbio zake katika wilaya ya Kibaha kwa kukagua na kuzindua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 ikiwa sehemu ya shughuli zilizofanywa na mbio wilayani Kibaha. Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI.HALIMA KIHEMBA akiwakabidhi wakimbiza mwenge wa uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe BIBI. FATMA KIMARIO, amebainisha kuwa miradi 11 imezinduliwa na kuweka jiwe la msingi katika wilaya ya Kibaha. BIBI.KIHEMBA amebainisha kati ya fedha hizo milioni 73 ni mchango wa halmashauri, milioni 49 mchango wa wananchi mchango wa wananchi, shilingi milioni 35 mchango wa wadau wengine, shilingi shilingi bilioni 1.5 ikiwa mchango wa serikali kuu. Mbio hizo zinaendelea katika wilaya ya Kisarawe ambapo huko unatarajia kukagua na kuweka mawe ya msingi kwa miradi mbalimbali thamani ya shilingi bilioni 1.4. Kauli mbiu ya mbio za mwenge mwaka huu ni TUSIKUBALI KUBAGULIWA KWA ITIKADI YA AINA YOYOTE, RANG...

MCHAKATO WA KATIBA.

KATIBA CHADEMA Ben Komba/Pwani-Tanzania/11:22/29-08-2013 Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha wamependekeza kuwa watumishi wote wa serikali wametakiwa kuorodhesha mali zao kabla ya kuanza kutumikia dhamana aliyopewa na nchi ili kutoa fursa kwa yeye kufilisiwa iwapo atatumia madaraka yake vibaya kwa kushiriki vitendo vya ubadhilifu. Akichangia hoja kuhusiana na rasimu ya Katiba, BW.ISIHAKA MNEMBWE ameomba kuingizwa kwa vifungu vitakavyowezesha wabadhirifu na mafisadi kufilisiwa iwapo watabainika kushiriki vitendo vya kinyume na utaratibu wa utumishi wa umma. BW.MNEMBWE amebainisha kuwa kuwaacha wabadhirifu wa mali ya umma bila kuchukuliwa hatua madhubuti ambazo zitawagusa moja kwa moja tatizo hilo litabaki kukomaa kutokana na wengine kuamua kufuata mkumbo kutakakosababishwa na kutochukuliwa hatua chanya ambazo zingeweza kuwatia hofu. Naye mchangiaji mwingine ambaye ni Katibu wa uchumi na Fedha wa CCM kata ya Janga, BW.OTTO KINYONYI amesema katiba mpya ihakikishe kuwa mali na fed...

WAFUGAJI NA WAKULIMA WAVUTANA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/27-08-2013/09:50 Wakulima wa katika Bonde la mto Ruvu katika kijiji cha Kidogozelo kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wameitaka halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kuwasaidia katika suala zima la kupambana na wafugaji wanaolisha katika mashamba yao na kuchoma moto vibanda vya shamba. Mkazi wa kijiji cha wakulima cha Kidogozelo BW. OMAR NDEKIO amesema kuwa wakulima wamekuwa wa desturi ya kuswagia mifugo yao katika mashamba ya wakulima kwa makusudi na inapotokea mkulima kulalamika wanamtishia. BW.NDEKIO amesema agost 22 mwaka huu Shamba lake la nyanya na mahindi lilivamiwa na ng’ombe na kuharibu kabisa mazao yake kwenye shamba, na kutokana na hilo alichukua hatua ya kwenda kuripoti Polisi Vigwaza ili kuangalia jinsi gani anaweza kufidiwa. Nikiongea na Mtendaji wa kijiji cha Wakulima cha Kidogozelo, BW.MANENO BUNA amesema yeye anayo taarifa kuhusiana na uvamizi uliofanywa katika shamba la BW. OMAR NDEKIO. Na mwandishi wa habari hizi alipotaka kuj...

WASAIDIWA MAFRIJI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-08-2013/17:59 Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini BW.SYLVESTER KOKA amewasaidia vijana wafanyabiashara wa stendi ya mabasi ya Mailimoja mjini Kibaha, mafriji mawili yenye thamani ya shilingi Milioni 1.5. Akikabidhi mafriji hayo kwa vijana hao, BW.KOKA amesema ametoa mafriji hayo kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana hao ambao wanajihusisha na kuuza maji ili waweze kupiga hatua katika biashara zao. BW.KOKA amesisitiza lengo ni kuhakikisha uchumi wa wananchi wa Kibaha mjini wanakuwa wana uchumi utakaowasaidia kupata ustawi wa kimaendeleo na amewakumbusha wana Kibaha kuhusiana na kauli aliyotoa wakati wa kampeni kuwa atawasaidia wananchi wote watakaounda vikundi. Amebainisha kupitia serikali ya CCM mpaka sasa wameshafanya mambo mengi ikiwamo uimarishaji wa miundombinu ya barabara na kuimarisha upatikanaji wa maji katika mji wa Kibaha. Mbunge huyo wa Kibaha mjini BW.SYLVESTER KOKA amewakumbusha juu ya kabla ya yeye kuwa mbunge katika kipindi ...

BARAZA LA KATIBA LA VIJANA KUFANYIKA KIBAHA

BARAZA LA VIJANA Ben Komba/Pwani-Tanzania/14:01/22-08-2013 Shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE-YPC- limeandaa mkutano wa Baraza la katiba la vijana wa wilaya ya Kibaha utakaofanyika kwa siku mbili na kuhudhuriwa na vijana 100. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, BW.ISRAEL ILUNDE amebainisha kuwa vijana watakaoshiriki ni pamoja na mabalozi wa YPC KUTOKA KATIKA Kata za halmashauri ya wilaya ya Kibaha, wanachama wa YPC kupitia vikundi vya wanawake vijana (WAVUMA) na wajumbe wa jukwaa la vijana Kibaha,KIBAHA YOUTH FORUM. Washiriki wengine wawakilishi vijana kutoka kwenye vikundi vya dini pamoja na asasi zingine za vijana na wadau wake, BW.ILUNDE amefafanua kuwa baraza hilo na vijana na wadau wataweza kutoa maoni yao, wakiwezeshwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, BW.DEUS KIBAMBA. Mkurugenzi huyo wa YPC, BW.ILUNDE amesema baraza hilo limeandaliwa kisheria chini ya kifungu cha 18(6) cha sheria ya mabadiliko ya katiba, sura ya 83 ambacho kinasemekana “Tume inaweza...

SIMBA WAJIPANGA PWANI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-8-2013/12:p30 Wanachama na washabiki wa SIMBA SPORTS CLUB katika Tarafa ya Miono wilaya ya Bagamoyo wameazimia kuanzisha Timu ya mpira wa miguu ambayo itakuwa tanurui la kuoka wachezaji kwa ajili ya kucheza timu ya wakubwa ya Simba katika suala zima la kuibua vipaji.   Mwenyekiti wa Tawi la Simba Mkubwa dawa lililopo mjini Bagamoyo, ABDUL SHARRIF amewaambia wana Simba wakati umefika kwa kutambua kuwa mpira ni ajira na si kitu cha kufanyia mzaha hata kidogo.   SHARRIF amebainisha kuwa Timu hiyo itakuwa chini ya MWALIMU. MTORO MAGOSO ambaye zamani amewahi kuichezea Simba, na kwa kuanzia ametoa nafasi kwa yoyote anayejua anaweza kusakata kabumbu kujitokeza ili kumpa nafasi Kocha kuweza kupata wachezaji stahili.   Ameitaka klabu hiyo kutosajili wachezaji kwa kufuata jina au uzuri ili kuepusha uwepo kwa mamluki katika timu hiyo kama ilivyotokea kwa mchezaji MRISHO NGASSA, amesema mpaka sasa tawi la Mkubwa Dawa limeshatoa wachezaji ...

MEYA SHARRIF AKEMEA UCHUKUAJI WA SHERIA MIKONONI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-8-2013/12:00 Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduz wilayani Bagamoyo, BW.ABDUL SHARIFF amewasaidia wakazi wa Mbwewe, Bagamoyo ambao nyumba zao sita zimechomwa moto kufuatia kutokea ajali ya gari eneo hilo na baadhi ya wakazi kukimbilia na kuiba mali zilizokuwamo kwenye gari. BW.SHARRIF ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya wananchi kuchukua sheria mikononi bila kuhusisha vyombo vya dola, amebainisha kuwa ameshuhudia nyumba hizo zilizochomwa moto na kusikitishwa na hali aliyokuta kutokana katika moja ya nyumba hizo kulikuwa na mgonjwa. BW.SHARRIF ameshangazwa na Polisi kuwashikilia wanakijiji 5 kwa kosa la kuiba mali katika gari lililopata ajali na wale waliochoma moto wakiachiwa huru na kutokana hali hiyo Mwenyekiti wa wazazi huyo ameahidi kufika eneo hilo siku ya Jumatatu katika kujua ukweli juu ya jambo hilo. Ameongeza kwa upande wake hafurahishwi na vitendo vyovyote vya uhalifu lakini wananchi hawana budi ...

AKAMATWA AKIBAKA MPWAWE.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/20-08-2013/10:25 Mkazi mmoja wa mjini Kibaha eneo la Mailimoja ,BW.SEBASTIAN MAGANGA amethibitika kukamatwa kwa kosa la ubakaji wa mwanafunzi mtoto wa mdogo wake. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia Mkaazi huyo akiwa ameongozana na kundi la watu ilihali akiwa mwili mzima umejaa damu akiwa na masikitiko makubwa kutokana na aibu. Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Pwani, Kamishna msaidizi ULRICH MATEI amebainisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mailimoja A, ambapo mtuhumiwa huyo ambaye ana mke alikuwa na desturi ya kuamka alfajiri kwenda kwa shangazi yake ambaye wakati huo uwa machinjioni na kumuingilia kimwili binti wa miaka 12 ambaye ni mwanae. Kutokana na kuwa na mazoea hayo ndipo siku ilipowadia aliponasa katika mtego uliotegwa na shangazi yake mtuhumiwa BIBI. CECILIA MABULA kutokana nay eye kupata taarifa hizo kuhusiana na mwenendo wa kushangaza wa BW.SEBASTIAN MAGANGA mabaye pia alikuwa Katibu mwenezi wa CCM kata ya Mailimoja. ...

KIFAA CHA KISASA CHA KUPIMA MWENDOKASI CHAWASILI.

WAENDESHA MAGARI KWA FUJO KUPATIKANA. Ben Komba/Pwani-Tanzania/15-08-2013/13:00 Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani limeanza majaribio rasmi ya kutumia kifaa cha kupima mwendo kasi kwa magari yanayotumia Barabara ya Morogoro ikiwa ni sehemu ya kupunguza ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara na kusababisha vifo na majeruhi. Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani katika mkoa wa Pwani, Mrakibu msaidizi wa NASSORO SISIWAYA amesema kifaa hicho ambacho kitakuwa kinatumia teknolojia ya kisasa itaweza kupunguza malalamiko yanayotolewa na madereva mara wanapokamatwa kutokana na kuendesha gari kwa mwendo kasi. Mrakibu msaidizi SISIWAYA amefafanua kutoka na kuja kwa kifaa hicho kipya cha kupima mwendokasi wa gari kinachotumia teknolojia ya kisasa na kinachotegemea kwa kiasi kikubwa mtandao wa intaneti ili kufanya kazi kwa usahihi. Ambapo kwa sasa askari wa usalama barabarani watapunguziwa adha ya kuanza kubisha na madereva wanaoendesha gari kwa fujo, kutokana na kifaa hicho kuwa na uwezo wa ...

WITO WATOLEWA KUSAIDIA YATIMA.

WATOTO YATIMA TUWASAIDIE Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-08-2013/10:02 Katika kuhakikisha jamii inawajali watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magummu, Mwenyekiti wa halmashauri ya mji mdogo wa Bagamoyo BW.ABDUL SHARRIF amezindua rasmi mfuko wao, katika kata ya Miono  wilayani Bagamoyo. Mwenyekiti huyo wa halmashauri BW.ABDUL SHARRIF ameitaka jamii kulipa kipaumbele suala la watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwapatia nafuu ya kupata baadhi ya mahitaji muhimu. Amebainisha kuwa yeye mwenyewe ametokea katika uyatima na anajua adha na machungu mbalimbali wanavyokumbana navyo watoto yatima katika maisha ya kila siku na kutokana na hilo akautaka uongozi wa Kata kuanzisha mfuko ambao utasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu. BW. SHARRIF kwa kuanzia alitoa shilingi laki tano kwa ajili ya ufunguzi wa akaunti ya mfuko huo wa kuwasaidia watoto yatima na akaahidi na mara baada ya akaunti hiyo kuanza kufanya kazi atawawekea shilingi mili...

HIFADHI MSITU RUVU KUSINI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/07-08-2013 Uharibifu wa hifadhi ya msitu Ruvu Kusini umepungua kufuatia doria kali za mara kwa mara zinazofanywa na idara ya Maliasili na utalii katika kuhakikisha wanazuaia ukataji wa miti holela unaotishia kuzuka kwa jangwa. Hivi Karibuni mwandishi wa habari hizi amejionea mwenyewe uharibifu unaofanywa na watu wanaojishughulisha na ukataji wa mkaa kinyume na taratibu na hivyo kutishia uoto wa asili wa hifadhi hiyo ya Ruvu Kusini. Mratibu wa mradi wa mama misitu unaonuia kulinda hifadhi yam situ wa Ruvu Kusini TFC, BW.YAHYA MTONDA  amebainisha katika hatua ambazo inabidi kuchukuliwa iwapo mtu atakutwa anakata mkaa bila kufuata taratibu ni kuporwa kwa baiskeli yake ambayo itabidi kulipa faini ili kuipata. Ameongeza kuwa kwa mtu yoyote anayekamatwa katika hifadhi anakabiliwa faini ya shilingi elfu sabini na aidha atawajibika kukilipa kijiji faini ya shilingi elfu 14 na hivyo kufanya jumla ya faini atakayolipa mtu aliyekiuka taratibu ni sh.e...

KOREA YASAIDIA KITUO CHA AFYA MKOANI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12:34/06-08-2013 Kituo cha afya mkoani katika halmashauri ya mji wa Kibaha kimepata msaada wa fedha zaidi ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuimarisha huduma ya afya ya mama na mtoto katika suala zima la kupunguza vifo vya watoto na kinamama wakati wa kujifungua. Akikabidhi hundi hiyo kwa Mganga mkuu wa mji wa Kibaha, BW.ISSA KANIKI, Balozi wa Korea nchini Tanzania BW.CHUNG LI amesema kuwa wameshawishika kutoa msaada huo kupitia shirika la misaada la Korea KOFIH, Ili kusaidia juhudi za serikali kupunguza vifo vya mama na watoto nchini. Balozi CHUNG LI amebainisha kuwa wao kwa upande wao wanapendelea kuona Tanzania inajitegemea katika suala la afya ya mama na motto ili kujenga Taifa lenye ustawi, ameyaseama kufuatia swali lililoulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na serikali yao itaendelea kusaidia Tanzania mpaka lini. Balozi CHUNG nchi yao imetoa kipaumbele kikubwa katika uimarishaji wa afya ya mama na mtoto ili kwenda sambamba na m...

FUTARI YATOLEWA KWA WAUMINI PWANI

Ben Komba/Pwani-TANZANIA/06-08-2013/13:27 Meya mji wa Bagamoyo ABDUL SHARIF amewataka Waislamu nchini kushirikiana na watu wenye imani tofauti katika kulijengea Taifa ustawi na kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania. BW.SHARIFU amesema hayo akitoa futari kwa wakazi wa eneo la Miono wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, amefafanua kuwa kumekuwa kuna wakijitokeza kujaribu kuanzisha migogoro ya kidini nchi mwetu ambayo haina tija yoyote kwa Watanzania, hivyo amewasihi Waislam kutokubaliana na uchonganishi huo unaotishia ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla. Amelaani baadhi ya wanasiasa wanaotumia mgongo wa dini kwa kujaribu kuanzisha vurugu nchini kwa lengo la kutaka kuendelea kutawala ilihali toka zamani wakristo na waislamu wote ni wa moja na wote ni watanzania. Naye Mbunge wa Kibaha mjini BW.SYLYVESTER KOKA naye ametoa futari kwa viongozi wa misikiti 56 iliyopo Kibaha ikiwa sehemu ya mchango wake kwa waumini wa dini ya kiislamu katika kipindi hiki cha mfungo w...