Posts

Showing posts from July, 2013

ZAO LA UYOGA MKOMBOZI KWA WAJASIRIAMLIA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13:21/25-07-2013 Wajasiriamali nchini wametakiwa kuwekeza katika zao la uyoga ili waweze kujiongezea kipato, katika suala zima la kukabiliana na maskini miongoni mwa jamii. Akiongea katika mafunzo yanayohusiana na kilimo cha zao la uyoga, Mtaalam PETRO MATHEW amebainisha kuwa iwapo wajasiriamli wakiamua kujikita katika kilimo cha zao wataweza kufaidika kiafya na kiuchumi. BW.MATTHEW amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwapatia mbinu na utaalamu wa kufanikisha uoteshaji wa uyoga katika mazingira ya nchi ya Tanzania, ambapo pia uzalishaji wake unasaidia kuweka mazingira katika hali safi, kutokana na kilimo chake kutumia zaidi takataka. Mtaalamu huyo BW.MATTHEW ameongeza kuwa uyoga ustawi katika takataka ambazo hazijaoza,takataka zilizooza kidogo na hata takataka zilizooza kabisa na hivyo kusababisha matumizi ya takataka kuchukua nafasi kubwa katika uzalishaji wa zao hilo. BW.MATTHEW ameelezea faida za uyoga ni pamoja na kuongeza kinga za mw...

MSASA POLISI JAMII.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013 Wananchi wametakiwa kutumiaulinzi shirikishi jamii kujiletea amani na utulivu katika maeneo kunakosababishwa na watu wanaoishi nao mtaani kwa kutoa taarifa katika suala zima la kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao. Mkuu wa Jeshi la Polisi mjini Kibaha, Mrakibu wa Polisi BAKARI KAWINGA amesema hayo wakati alipokutana na polisi jamii katika kata ya Pangani ambapo amefurahishwa kwa Kata hiyo kuwa na matukio kidogo ya uhalifu, kulinganisha na kabla ulinzi huo haujanzishwa. BW.KAWINGA amebainisha kuwa iwapo umebahatika kuwa Polisi jamii, basi ni vyema kutumia fursa hiyo katika kutenda haki bila kubugudhi wengine kwa kisingizio cha kuwa na namba za simu za wakuu wa Jeshi hilo wa Mkoa wa Pwani. BW.KAWINGA ameongeza kuwa Jeshi la Polisi lina nia njema ya kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kushirikiana na wananchi ambao watakuwa na wajibu wa kutoa taarifa wanapoona kuna jambo la kutia mashaka katika mitaa yao. Aidha ...

MAFUNZO YA UREFA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013/10:03 Chama cha marefa wilayani Kibaha kinaendesha program maalum ya mafunzo kwa marefa wapya wenye kutaka kujiendeleza kuwa waamuzi katika ngazi mbalimbali za ligi za mchezo huo. Katibu wa Chama cha marefa wilayani Kibaha ambaye pia ndio refa bora wa ligi ya VODACOM msimu uliopita BW.SIMON MBELWA amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha kuzalisha marefa wapya. BW.MBELWA amefafanua kuwa katika mambo ambayo yatazingatiwa katika mafunzo hayo ni ufundishaji wa sheria 17 za soka ambazo kila mwamuzi anapaswa kuzifahamu kwa ufasaha ili kuepusha malalamiko na wakati mwingine hata vurugu katika mchezo huo. Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, BW. GEORGE amesema kwa kupatiwa mafunzo hayo kutawasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi wakati wakichezesha mechi za michuano mbalimbali. END.

SKAUTI WAAPISHWA KIBAHA.

MASKAUTI ST.DON BOSCHO WAAPISHWA Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/11:36 Maskauti nchini wametakiwa kuenenda na maisha ya uskauti katika kipindi cha maisha yao yote ili waweze kuishi maisha ya ukakamavu utii na unyenyekevu ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii. Ameyaongea hayo Padri.FULGENCE RUTATEKURURWA wakati wa uapishaji wa maskauti kutoka shule ya ST.DON BOSCHO mjini Kibaha na kuhudhiriwa na maskauti wenzao kutoka nchini USWISSI. PADRI.RUTATEKURURWA amewataka maskauti hao kuishi maisha ya kiskauti na kuwa changamoto kwa wenzao,ili waweze kujiunga na skauti hivyo ni fursa waliyopewa kama maskauti wapya kuhamasisha wenzao kujiunga nao. Na amewataka kuambatana na kiapo chao ili waweze kutoa huduma hiyo kwa kufuata kanuni na miongozo ya skauti aidha amewakumbusha mara mtu unapokuwa skauti basi unakuwa skauti milele. Naye Kamishna msaidizi wa skauti mkoa wa Pwani, Skauta ANTHONY MWENDA  Amesema lengo la hafla hiyo ni kuapisha maskauti wapya wa ST.DON BOSCHO ambao...

BONANZA LA MICHEZO KWA WANAWAKE KKKT.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/11:06 Wanawake wakristo nchini wamehimizwa kushiriki Bonanza la michezo  kwa wanawake wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ambayo itakuwa inafanyika kila baada ya klipindi Fulani katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha. Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Bonanza hilo, BIBI. VERONICA KILEO amesema kuwa ni mara yao ya kwanza kuandaa bonanza hilo kwa lengo la kuhamasisha kinamama washiriki michezo. BIBI.KILEO amefafanua kuwa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambayo ina kanda za kiusharika sita ndio zilizotakiwa kushiriki mashindano hayo lakini hata hivyo ni kanda nne tu zilizoshiriki Bonanza hilo, na kanda mbili za Zanzibar na magharibi zikishindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali. BIBI.KILEO ameongeza kuwa michezo mbalimbali imeshindaniwa katika bonanza hilo ikiwa pamoja na mazoezi kupasha mwili moto (warmup) kwa takriban dakika 15,kukimbiza kuku, kuvuta kamba na mpira wa pete. Mshauri wa kamati ya maandalizi ya Bo...

KATIBU CCM AONYESHA UKOMAVU WA KISIASA.

KATIBU CCM KIBAHA MJINI ASHANGILIWA NA BAVICHA. Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/10:27 Katibu wa Chama cha Mapinduzi mwishoni mwa wiki amejikuta akipigiwa makofi na wananchama wa chama cha maendeleo na demokrasia wa mjini Kibaha baada ya kujitokeza na kusuluhisha mvutano uliopo wa kuzuia CHADEMA kufungua matawi katika maeneo mbalimbali mjini Kibaha. Mwandishi wa habari hizi alishuhudia Katibu wa CCM Kibaha mjini, BIBI.MWAJUMA NYAMKA akitoka ofisini kwake akaenda moja kwa moja kwenye kundi la vijana wa CHADEMA ambao katika kipindi hicho walikuwa wanavutana na Diwani wa CCM kata ya Mailimoja, BW.ANDREW LUGANO ambaye alikuwa akizuia ujenzi huo. Ambapo BIBI.NYAMKA kwa kutumia busara nadra sana kuonyeshwa na viongozi wa kisiasa, alimtaka diwani huyo kuwaacha waendele kufungua matawi kwani kinachoangaliwa na wananchi ni sera sio wingi wa matawi. Naye Diwani wa Kata ya Maili moja kupitia tiketi ya CCM, BW.ANDREW LUGANO yeye kwa upande wake amezuia ujenzi holela wa matawi ya C...

HABARI ZA POLISI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI   Kibaha tarehe 19 Julai, 2013 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoa wa Pwani imemuhukumu Bw. Amosi Mwita Chacha umri miaka 40, Mkazi wa Miembe Saba Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwenda jela miaka 6 baada ya kukutwa na hatia katika Kesi ya Wizi wa vocha za tigo pamoja na kesi ya Kukutwa na Mihuri bandia. Mtuhumiwa huyo amekutwa na hatia kwa makosa yote mawili yaliyokuwa yakimkabili Katika kesi iliyokuwa ikisikilizawa na Hakimu Mkazi, Mhe. Aziza Mbadyo. Mwendesha mashitaka wa Serikali Bw. Emmanuel Maleko   ameeleza mbele ya   mahakama kuwa mtuhumiwa mnamo tarehe 03 Juni 2013 huko eneo la Sinza Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam alikutwa akiwa na Mihuri ya Afisa Mtendaji Mtaa wa kwesimu pamoja na wa Kituo cha Ukaguzi wa Maliasili cha Soni kilichopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mihuri hiyo katika usafirishaji wa mali asili kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam kwa ...

MADHARA YA MITANDAO

Ben Komba/13:30/19/07/2013. Matumizi ya mtandao yamekuja na changamoto zake ambazo zimesababisha kasi mpya ya mmonyoko wa maadili katika jamii, kutokana na baadhi ya watu kutumia mitandao hiyo kinyume na taratibu zinazongatia ustaarabu na maadili. Katika tukio moja mwanadada TAUSI SHAABAN mkazi wa mjini Kibaha amejikuta katika wakati mgumu kufuatia rafiki yake ambaye amesoma nae shule ya msingi kumchafua kupitia mtandao wa kijamii PEPERONITY. Bint. SHAABAN amesema kijana huyo ambaye amefanya hivyo anamkumbuka kwa jina moja la BARAKA ambaye kwa sasa anaishi Mwanza ambaye kwa mara ya mwisho alikutana naye Kituo cha Mabasi ya mkoani Ubungo ambapo kijana huyo alimuomba namba yake ya simu. Na wakati wakibadilishana namba hizo, Kijana alimuuliza Bint. Shaaban kama ameshazaa na alipojibiwa ndipo alipoaanza kumwambia maneno ya kuudhi na kejeli na kumuahidi kuwa atamkomesha, na ndipo jana ghafla akaanza kupokea simu kutoka kwa wanaume wakware. Bint. Shaaban ameongeza ...

WANANCHI WATAKIWA KUACHA SHAMBA LA MWENYEWE.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Thursday, July 18, 2013 Mkuu wa wilaya ya Kibaha BI.HALIMA KIHEMBA amewataka wakazi ambao wanasemekana kuvamia eneo la BW. MOHAMED SUMA kuondoka mara moja ili kutoa fursa kwa mmiliki kuliendeleza. Akiongea na wakazi wa Mtakuja katika kata ya Pangani halmashauri ya mji wa Kibaha BI.KIHEMBA ambaye ameshafika katika eneo hilo mara tatu katika suala zima la kujaribu kutafuta suluhu kati ya mmiliki na wakazi ambao wanasemekana wamevamia. BI.KIHEMBA akisoma barua iliyotoka kwa kwa mmiliki wa shamba hilo, BW.MOHAMED SUMA ambayo imefafanua kuhusiana na watu ambao yeye amewakabidhi eneo la heka 16 kwa watu wanane kila mmoja heka 2. Kwa hatua hiyo BI.KIHEMBA amewasihi wakazi hao kuondoka katika eneo hilo toka wanaokaa eneo hilo wanadai wamepewa bure hivyo amewataka nao kurudisha eneo hillo bure ili kuondoa usumbufu kwa ofisi yake. Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtakuja BW. LONGINO KASONTA amesema mzigo mkubwa anasukumiziwa yeye il...

VUTA NIKUVUTE CDM/CCM PWANI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14:23/17/7/2013. cha Demokrasia na maendeleo kimelalamikia hatua ya viongozi wa halmashauri kuwazuia kujenga matawi ya chama hicho katika lengo zima la kutekeleza ilani ya chama chao. Diwani wa Kata ya Tumbi, BW. MBENA MAKALA amesema hayo kufuatia vuta nikuvute kati yao na watu wanaodaiwa kutumwa na wakubwa kusitisha ujenzi wa tawi lao ikiwa sehemu ya utekelezaji wa kazi zao za siasa. Bw. MAKALA amebainisha kuwa imekuwa vigumu kwao wanapotaka kujenga matawi ya chama cha chao kwa madai ya kuwa wanahitajika kuwa na vibali vinavyowaruhusu kujenga. Ambapo BW.MAKALA amebainisha kuwa imekuwa tofauti na wenzao wa chama tawala ambao wamekuwa wakijenga mashina ya wakereketwa na matawi bila kusumbuliwa na vyombo vya dola, na kuichukulia hali hiyo kama ukandamizaji wa demokrasia nchini. Diwani huyo alishangazwa na diwani wa CCM kata ya Mailimoja BW.ANDREW LUGANO  kujaribu kusimamisha ujenzi wa tawi hilo kwa madai ya kutekeleza maagizo kutoka kwa wa...

ABIRIA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO SUMATRA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/7/2013,10:36 Mamlaka ya ya usafiri wa majini baharini na nchikavu imewataka abiria kushirikiana kwa karibu na malamka inapotokea ukiukaji wa taratibu za usafiri unaofanywa na wamiliki na wafanyakazi wa magari ya abiria. Akiongea na mwandishi wa habari hizi afisa mfawidhi mkuu wa SUMATRA Mkoa wa Pwani, BW.NASHON IROGA amesema kumekuwepo na matatizo makubwa wanayokabiliana nayo katika kuhakikisha huduma za usafiri zinazotolewa zinakuwa katika kiwango stahili. BW.IROGA amesikitishwa na baadhi ya abiria ambao wamekuwa wanashirikiana na wafanyakazi wa magari ya abiria kukiuka kwa makusudi taratibu za usafiri salama na hata kushirikiana nao inapotokea bai limeshikiliwa kutokana kukiuka taratibu kwa kisingizio cha kutaka kufika wanapokwenda. Naye msafiri alikuwa anasafiri na na Basi la Mbazi aliyejulikana kwa jina la YUDA kwa upande wake amesikitishwa na kitendo cha nauli kupandishwa kiholela kwa abiria huku mamlaka husika zikiwa hazichukui h...

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUCHANGIA JAMII.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/09:46/09/07/2013. Wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa nchini wameshauriwa kuwa na utamaduni wa kusaidia taasisi mbalimbali za kijamii katika suala zima la kuaharakisha maendeleo ya nchi na wananchi wenyewe. Hayo yamezungumzwa na mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini, BW.SYLVESTER KOKA wakati akikabidhi msaada wa madawati 50 kwa shule za msingi Jitihada na Lulanzi yaliyotolewa na taasisi ya mikopo kwa wafanyakazi wa umma FAIDIKA. BW.KOKA amesema kwa jinsi anavyofahamu uwepo wa wafanyabiashara wenye fedha nyingi ambao wangefuata nyayo za Taasisi ya FAIDIKA wangeweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Amebainisha kwa sasa nchi yetu ina wafanyabiashara mbalimbali wakubwa ambao kama wangekuwa wanatoa asilimia hata 5 ya walicho nacho katika kuchangia shughuli za kijamii basa kero nyingi za kijamii zingepungua hususan upande wa elimu. Mwakilishi wa Mkurugenzi wa taasisi ya mikopo ya FAIDIKA, BW.HARUN FERUZ amesema taasisi yake imekuwa na utamaduni...

KABURI LABAKI WAZI KULIKOSABABISHWA NA UTAPELI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/31/6/2013/09:45 Katika kile kinachoashiria kuwa heshima na utu wa mwanadamu unaporomoka kwa kasi, Mtanzania mmoja anayejulikana kwa jina la ABDUL RAMADHAN amefanya vitendo vya kitapeli kwa jamii ya waislamu wanaoishi katika maeneo ya Kibaha kwa Mathias mjini Kibaha. Inasemekana kuwa siku ya Jumapili BW.ABDUL RAMADHAN alifika maeneo ulipo msikitini kwa lengo la kutaka usaidizi wa kumzika mtu ambaye alikuwa mfanyakazi wake wa nyumbani ambaye amefariki. BW.RAMADHAN alimwambia Imamu SAID OMAR wa msikiti QADIRIYA kuwa yeye alikuwa anaishi na marehemu kama mfanyakazi wa nyumbani lakini kwa bahati mbaya mauti yamemkuta na hivyo angehitaji msaada wao ili kuweza kwenda kumsitiri marehemu. Baada ya kumsikiliza kwa makini Tapeli huyo ambaye uso wake ulionyesha kila dalili za masikitiko na uchungu usio kifani alipatiwa msaada ambao aliutaka ikiwa pamoja na wachimba kaburi ambao walifanya kazi yao kwa ufasaha. Ndipo wakati ukafika akamwambia Imam OMAR w...