WABUNGE WAHITIMU MAFUNZO 832 KJ.
WABUNGE WAHITIMU MAFUNZO 832 KJ. Ben Komba/Pwani-Tanzania/29-Mar-13/09:46:30 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, DKT. JAKAYA KIKWETE amekumbuka ujasiri ambao aliupata kutokana na yeye kupitia Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria,akiwa katika kombania C ambapo alikutana na watu mbalimbali na kupata uzoefu mkubwa wa kimaisha. DKT. KIKWETE amebainisha kutokna na kupitia kwa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria na kubahatika kupangiwa katika kikosi cha 832 cha Jeshi la kujenga Taifa Ruvu, na amewapongeza wabunge ambao wamehitimu mafunzo yao ya wiki tatu kwa kuonyesha uzalendo. Katika ziara hiyo Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, DKT. JAKAYA KIKWETE ametembelea maeneo mbalimbali ya miradi ya kikosi na kuona nyumba namabweni ya vijana wa JKT na kufunga mafunzo maalum ya JKT kwa wabunge ambao wamehudhuria mafunzo hayo ambayo yalianza March 4. Wabunge ambao wamehudhuria mafunzo hayo ni, BW.DAVID SILINDE, BW. MURTAZA MANGU...