Posts

Showing posts from February, 2016

VIDEO-WANANCHI WASULUBIWA KUTOKANA NA ITIKADI ZA SIASA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/29/2016 3:04:50 PM Wananchi katika kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo wamelalamikia kitendo cha Chama Tawala kuwabagua kwa kufuata misingi ya kisiasa. RFA imegundua hilo kufuatia kuzuru kijiji hicho cha Kitonga, Ambapo mmoja wa wanachama wa Chama shindani, BW. FADHILI KUNGULWE amesema kuwa kumekuwepo na hujuma mbalimbali ambazo zimekuwa zinfanywa na Chama tawala. BW.KUNGULE amebainisha kuwa wananchama wa vyama shindani katika kijiji hicho wamekuwa wanaishi katika maisha ya dhiki kufuatia Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Kitonga, BW. MOHAMED KIGUMI kutumia nafasi yake kukandamiza wananchi ambao hawaungi mkono chama tawala. Nilipotaka kujua kwanini wananchi wameigeuka CCM, BW. KUNGULWE amefafanua kuwa kikubwa ni mchakato wa kuwapata wagombea mbalimbali katika uchaguzi mkuu na ikiwa pamoja na kushindwa kuwajibika katika kukiletea maendeleo ya kijiji. Naye mwananchi mwingine BW,KHALIFA MGALAMO ameongeza kuwa uo...

WANANCHI WALALAMIKA KUBAGULIWA KWA MISINGI YA KISIASA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/29/2016 3:04:50 PM Wananchi katika kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo wamelalamikia kitendo cha Chama Tawala kuwabagua kwa kufuata misingi ya kisiasa. RFA imegundua hilo kufuatia kuzuru kijiji hicho cha Kitonga, Ambapo mmoja wa wanachama wa Chama shindani, BW. FADHILI KUNGULWE amesema kuwa kumekuwepo na hujuma mbalimbali ambazo zimekuwa zinfanywa na Chama tawala. BW.KUNGULE amebainisha kuwa wananchama wa vyama shindani katika kijiji hicho wamekuwa wanaishi katika maisha ya dhiki kufuatia Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Kitonga, BW. MOHAMED KIGUMI kutumia nafasi yake kukandamiza wananchi ambao hawaungi mkono chama tawala. Nilipotaka kujua kwanini wananchi wameigeuka CCM, BW. KUNGULWE amefafanua kuwa kikubwa ni mchakato wa kuwapata wagombea mbalimbali katika uchaguzi mkuu na ikiwa pamoja na kushindwa kuwajibika katika kukiletea maendeleo ya kijiji. Naye mwananchi mwingine BW,KHALIFA MGALAMO ameongeza kuwa uong...

VIDEO-AFISA MTENDAJI ATUKANA KIJIJI KIZIMA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/26/2016 3:47 PM Wanakijiji wa kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo wamekerwa na tabia ya afisa mtendaji wa kijiji hicho kutukana wananchi kufuatia mkutano wa wazi ambao umefanyika  kijijini hapo na kumshirikisha mkuu wa wilaya Bagamayo hivi karibuni. Wakizungumza na mwandishi wa RFA Pwani, Mmmoja wa wakazi hao BW.SAID ABDALLAH  amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya Mwenyekiti wa Kijiji kushindwa kumchukulia hatua afisa mtendaji huo na kwenda  kutoa ushahidi wa uongo mahakamani. BW.ABDALLAH ameongeza kuwa baada ya Afisa mtendaji kutukana kijiji kizima na kutishia kuwakamata kuwapeleka jele kwa ajili ya kwenda kufanywa kinyume na maumbile hivyo kufanya wazee wa kijiji hicho kutaharuki na kuamua kuchukua hatua za kisheria ambapo alipofika kule akisaidiwa na mwenyekiti wa kijiji hicho alishinda kesi kitu ambacho wananchi hawakukubaliana nacho na hivyo kutaka viongozi hao waondolewe katika nafasi zao. Kadhia hiyo ...

VIDEO-VIGOGO WAVAMIA MSITU MOROGORO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/27/2016 11:56:43 AM Wananchi wamesisitizwa kufuata sheria zilizopo zenye kulinda hifadhi za misitu ili kuboresha mazingira ya nchi na kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi ambako kunasababishwa na ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya shughuli za kibinadamu. Mshauri wa maliasili Mkoa wa Morogoro BW.JOSEPH CHUWA ameyazungumza hayo hivi karibuni OFISINI KWAKE kufuatia kuongezeka kwa uvamizi wa maeneo ya hifadhi na kusababisha kuongezeka kwa utokaji wa hewa ukaa ambayo inaathiri majira ya mwaka. BW.CHUWA amesema iwapo kila mmoja wetu akiheshimu sheria za uhifadhi wa misitu kama ilivyoanishwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudisha hifadhi za misitu na kurudi kama awali. Moja ya hifadhi ya misitu iliyovamiwa ni iliyopo kati ya wilaya ya Mvomero na manispaa ya mji wa Morogoro na watu kuanzisha makazi na wengi wao kuwa ni vigogo wenye nafasi mbalimbali katika serikali na vyama ikiwa pamoja na matajiri. Ambapo kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi ...

AFISA MTENDAJI KITONGA BAGAMOYO ATUKANA KIJIJI KIZIMA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/26/2016 3:47 PM Wanakijiji wa kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo wamekerwa na tabia ya afisa mtendaji wa kijiji hicho kutukana wananchi kufuatia mkutano wa wazi ambao umefanyika  kijijini hapo na kumshirikisha mkuu wa wilaya Bagamayo hivi karibuni. Wakizungumza na mwandishi wa RFA Pwani, Mmmoja wa wakazi hao BW.SAID ABDALLAH  amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya Mwenyekiti wa Kijiji kushindwa kumchukulia hatua afisa mtendaji huo na kwenda  kutoa ushahidi wa uongo mahakamani. BW.ABDALLAH ameongeza kuwa baada ya Afisa mtendaji kutukana kijiji kizima na kutishia kuwakamata kuwapeleka jele kwa ajili ya kwenda kufanywa kinyume na maumbile hivyo kufanya wazee wa kijiji hicho kutaharuki na kuamua kuchukua hatua za kisheria ambapo alipofika kule akisaidiwa na mwenyekiti wa kijiji hicho alishinda kesi kitu ambacho wananchi hawakukubaliana nacho na hivyo kutaka viongozi hao waondolewe katika nafasi zao. Kadhia hiyo im...

WAZIRI SIMBACHAWENE AAHIDI KUSHUGHULIKIA KERO SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania2/21/2016 10:28 AM Shirika la elimu Kibaha limetakiwa kufanyakazi kwa kadiri ya misingi ya uanzishwaji wake ili liweze kufikia malengo yalikusudiwa. Hayo yamezungumzwa na Waziri wan chi ofisi ya Rais TAMISEMI,BW.GEORGE SIMBACHAWENE wakati akizungumza akiwa katika ziara ya kutembelea shirika hilo mjini Kibaha. Ambapo amesema kuwa kwa kufuta misingi ya kuanzishwa kwake ambako kulikuwa kumelenga kumkomboa mwananchi wa kijijini kutoka kwa maadui wakuu watatu ujinga,maradhi na umaskini katika kuhakikisha maendeleo yanafika hadi ngazi ya kijiji. Aidha katika ziara yake ametembelea mradi wa mwekezaji ORGANIA ambao wamewekeza katika mifugo na kilimo na kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi huo. Jambo jingine ambalo Waziri SIMBACHAWENE alikutana nalo ni malalamiko ya wafanyakazi ya kuwepo kwa kukosa stahili zao mbalimbali ambapo waziri huyo amewaahidi wafanyakazi kuzichunguza na kutoa mrejesho kwao hapo uchunguzi utakapokamilika. Kwa upande...

VIJANA WATAKIWA KUGANGAMALA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/21/2016 11:56:15 AM Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI. HALIMA KIHEMBA ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidiana na serikali katika kuhakikisha vijana wanatambua wajibu wao. Ameyasema wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa utekelezaji wa taasisi ya YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ambao umelenga katika uhamasishaji wa vijana katika kujitegemea kiuchumi. BIBI.KIHEMBA amesema ni wajibu wa vijana wenyewe kuwajibika katika maeneo yao ikiwa pamoja na kutatua kero zinazowazunguka ikiwa sehemu ya uungaji mkono harakati za Rais Magufuli katika kuhakikisha Taifa linapiga hatua za maendeleo. Naye mwakilishi mkazi wa Taasisi inayosaidia ukuaji wa demokrasia kutoka nchini Marekani NATIONAL DEMOCRATIC INSTITUTE, BW. BODURIN ADEBO amebainisha kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia mashirika yasiyo ya kiserikali katika masuala mazima ya utoaji wa elimu ya uraia katika kuimarisha demokrasia na utawala bora katika maene...

VIGOGO MORO WAVAMIA HIFADHI YA MSITU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/21/2016 1:27:25 PM Wananchi wamesisitizwa kufuata sheria zilizopo zenye kulinda hifadhi za misitu ili kuboresha mazingira ya nchi na kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi ambako kunasababishwa na ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya shughuli za kibinadamu. Mshauri wa maliasili Mkoa wa Morogoro BW.JOSEPH CHUWA ameyazungumza hayo hivi karibuni OFISINI KWAKE kufuatia kuongezeka kwa uvamizi wa maeneo ya hifadhi na kusababisha kuongezeka kwa utokaji wa hewa ukaa ambayo inaathiri majira ya mwaka. BW.CHUWA amesema iwapo kila mmoja wetu akiheshimu sheria za uhifadhi wa misitu kama ilivyoanishwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudisha hifadhi za misitu na kurudi kama awali. Moja ya hifadhi ya misitu iliyovamiwa ni iliyopo kati ya wilaya ya Mvomero na manispaa ya mji wa Morogoro na watu kuanzisha makazi na wengi wao kuwa ni vigogo wenye nafasi mbalimbali katika serikali na vyama ikiwa pamoja na matajiri. Ambapo kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi...

VIDEO=WANANCHI WATUMIE SHERIA NDOGO KULINDA MISITU

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/12/2016 10:45:20 AM Wananchi wanaoishi kupakana na msitu wa Ruvu Kusini wametakiwa wasiogope kutumia sheria ndogondogo ambazo wamejiwekea katika suala zima la kulinda misitu ya hifadhi na kuboresha mazingira  yanayowazunguka. Akizungumza ofisini kwake Meneja misitu  wa Kanda ya mashariki, BW. BAKAR MOHAMED amezungumza hayo alipokutana na waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Kibaha amewasisitiza wananchi kutumia sheria zao ndogondogo walizotunga wenyewe katika kulinda misitu ya hifadhi. BW.MOHAMED ameongeza  kuwa mkanganyiko wa gawio kwenda serikali iwapo wanakijiji wamekamata maharamia wa mazao ya misitu, faini au adhabu  yoyote itatolewa na kamati ya kijiji cha mazingira na fedha kuingizwa katika mfuko wa kijiji. Toka sheria hizo ndogondogo zzimetungwa kukidhi matakwa ya kijiji husika na hivyo kipato chochote kitachopatikana katika usimamizi wa misitu ya hifadhi hususan ya kijiji hakutakuwa na gawio kupeleka serikali...

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA SHERIA NDOGONDOGO ZA MISITU KULINDA HIFADHI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/12/2016 10:45:20 AM Wananchi wanaoishi kupakana na msitu wa Ruvu Kusini wametakiwa wasiogope kutumia sheria ndogondogo ambazo wamejiwekea katika suala zima la kulinda misitu ya hifadhi na kuboresha mazingira  yanayowazunguka. Akizungumza ofisini kwake Meneja misitu  wa Kanda ya mashariki, BW. BAKAR MOHAMED amezungumza hayo alipokutana na waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Kibaha amewasisitiza wananchi kutumia sheria zao ndogondogo walizotunga wenyewe katika kulinda misitu ya hifadhi. BW.MOHAMED ameongeza  kuwa mkanganyiko wa gawio kwenda serikali iwapo wanakijiji wamekamata maharamia wa mazao ya misitu, faini au adhabu  yoyote itatolewa na kamati ya kijiji cha mazingira na fedha kuingizwa katika mfuko wa kijiji. Toka sheria hizo ndogondogo zzimetungwa kukidhi matakwa ya kijiji husika na hivyo kipato chochote kitachopatikana katika usimamizi wa misitu ya hifadhi hususan ya kijiji hakutakuwa na gawio kupeleka serikali k...

VIDEO-MAAFISA MISITU WATAKIWA KWENDA NA KASI YA MAGUFULI

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/7/2016 12:45:29 PM Wajumbe wa kamati za mazingira wa vijiji vinavyopakana na Msitu wa Ruvu Kusini kutoka wilaya za  Kibaha na Kisarawe zimeunda kamati ya pamoja ambayo itakuwa na wajibu wa kuhakikisha wanashirikiana na ofisi  ya misitu  wilaya katika kuhakikisha mikataba mbalimbali inayohusiana na misitu inatiwa saini kuwa sheria. Akizungumza katika majumuisho ya mafunzo ya kuchambua mwongozo rahisi wa usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja  kwa ajili ya ushirikishwaji wa jamii katika usimamizi wa misitu ya hifadhi, BW.CASSIAN SIANGA amesema kupitia kampeni ya MAMA MISITU wameweza kutafsiri mwongozo hu ambao utazipatia kamati za mazingira za vijiji meno. BW.CASSIAN amebainisha kuwa usimamizi shirikishi wa misitu(USM) ni neno la jumla ambalo linaelezea ushiriki wa jamii katika usimamizi wa misitu, ambapo  kuna aina mbili za ushiriki ambazo ni usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja ambao unafanywa kwenye ardhi y...

KAMATI ZA MISITU ZAPEWA MENO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/7/2016 12:45:29 PM Wajumbe wa kamati za mazingira wa vijiji vinavyopakana na Msitu wa Ruvu Kusini kutoka wilaya za  Kibaha na Kisarawe zimeunda kamati ya pamoja ambayo itakuwa na wajibu wa kuhakikisha wanashirikiana na ofisi  ya misitu  wilaya katika kuhakikisha mikataba mbalimbali inayohusiana na misitu inatiwa saini kuwa sheria. Akizungumza katika majumuisho ya mafunzo ya kuchambua mwongozo rahisi wa usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja  kwa ajili ya ushirikishwaji wa jamii katika usimamizi wa misitu ya hifadhi, BW.CASSIAN SIANGA amesema kupitia kampeni ya MAMA MISITU wameweza kutafsiri mwongozo hu ambao utazipatia kamati za mazingira za vijiji meno. BW.CASSIAN amebainisha kuwa usimamizi shirikishi wa misitu(USM) ni neno la jumla ambalo linaelezea ushiriki wa jamii katika usimamizi wa misitu, ambapo  kuna aina mbili za ushiriki ambazo ni usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja ambao unafanywa kwenye ardhi ya misi...