BODABODA WAPATIWA MAFUNZO
Ben Komba/Pwani-Tanzania/8/31/2015 4:55:15 PM Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani limewatunuku vyeti madereva wa bodaboda ambao wamemaliza mafunzo ya usalama barabarani ambayo yametolewa na shirika lisilo la kiserikali la ANTI POVERTY AND ENVIROMENTAL CARE-APEC. Mkurugenzi wa shirika hilo, BW.RESPICIUS TIMANYWA ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha usalama wa vyombo hivyo linakuwa jambo la lazima kwa kutoa elimu ambayo ikizingatiwa itaweza kuokoa maisha ya wengi. Bw.TIMANYWA amefafanua kuwa mpaka sasa wameshafikia mikoa 15 katika kuhakikisha wanawajen gea uwezo madereva kiuchumi na kijamii na kufanikiwa kupunguza ajali kwa asilimia 95 ya wale ambao wamepatiwa mafunzo. Mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi TABITHA MAKARANGA amewashukuru APEC kwa kutoa mafunzo hayo ambayo kwa njia moja au nyingine yataweza kupunguza ajali zinazosababishwa na bodaboda. Mrakibu mwandamizi MAKARANGA amesema kuwa takwimu mpaka sasa zinaonyesha waathirika wakubwa wa ajali za ...