VIDEO-WANANCHI WALALALMIKIA SERIKALI KUWAUNGA MKONO WAVAMIZI WA ARDHI.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/7/9/2015 1:19:31 PM
Wananchi wa mtaa wa Kiluvya A,kata ya Kiluvya tarafa ya Sungwi wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani wametaka vyombo vinavyohusika na utoaji haki wa kisheria kushugulikia mgogoro wa ardhi yenye ukubwa wa heka 338 walizoporwa na wanaodaiwa wawekezaji.

Mmoja wa wakazi wa Kiluvya, BW.ABUBAKAR YUSSUPH amesema kama wamiliki wa maeneo yaliyovamiwa ambao mpaka sasa wamekuwa wakizungushwa pamoja na suala hilo kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.

BW.YUSSUPH ameeleza kutoridhishwa na mwenendo wa kesi ya kuporwa ardhi na uongozi wa kijiji na kupewa mabepari, kwa njia ya kughushi nyaraka na kilio cha kikubwa ni Polisi kuchelewesha kupeleka vielelezo kwa mwendesha Mashtaka wa serikali kanda ya Pwani.

BW.YUSSUPH amefafanua kuwa kesi hiyo imedhoofishwa kwa makusudi ili kutoa fursa kwa wavamizi kuchukua eneo hilo ambao idadi yao ni 15 na wanababaisha watu 250 na mamlaka husika zinajua kuhusiana na hilo.

Naye mkazi wa Mtaa wa Kiluvya, BIBI.ALFREDINA RAPHAEL amesema yeye amekaa eneo hilo toka mwaka 1972, Lakini kumejitokeza watu ambao wanadai kuwa eneo hilo ni lao na walikuwa wanaharakati ya kutaka kumiliki eneo hilo kutokana tu wao wana fedha.

BIBI.RAPHAEL ameshangazwa na serikali na CCM ambao wanajua kinaga ubaga kuhusu nani ana haki ya kumiliki eneo hilo, lakini kutokana na rushwa viongozi wamekuwa wakifumbia macho mgogoro huo.

 BIBI.RAPHAEL ameongeza kuwa mpaka sasa hatima yao haijulikani hasa kwa viongozi wao ambao wamewateua kufuatailia suala hilo ili kufahamu ukweli wa ambao upo bayana, ingawa wavamizi kwa kushirikiana na viongozi  wanataka kupotosha ukweli.

Nilipata bahati ya kuongea Mmoja wa wanaolalamikiwa kati ya watu 15 wanaodaiwa kuvamia eneo hilo kinyume cha taratibu, BW.ZEDI ABDUL ambaye kwa upande wake amesema kuwa eneo hilo wamelinunua kutoka kwa BW.SAID BAKARI MAZOEA.


BW.ABDUL  amesema yeye na wenzie wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kuanza upimaji ndipo wananchi walipojitokeza na kuzuia zoezi hilo, hali ambayo limewasababishia hasara kubwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA