SERIKALI YATAKIWA KUWAJENGEA UWEZO WAJASIRIAMALI.
Wananchi wametakiwa
kuwa makini katika kuhakikisha nchi inafikia malengo ya maendeleo endelevu ili kujikwamua
na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazowakabili hususan ya kiuchumi.
Mwezeshaji kutoka
shirika lisilo la kiserikali la -YPC-YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE ambalo limeandaa
semina hiyo kwa kushirikiana na ACTION AID , BW.SAMUEL STANLEY amesema lengo la
Semina hiyo ni kuutambulisha mradi wa ViVA yaani sauti za vijana kwenye uwajibikaji.
BW.STANLEY
amesema kupitia mradi huo wanategemea kuwajengea uwezo vijana na wananchi kwa ujumla
kutambua nafasi yao katika kuchoche uwajibikaji katika vijiji na vitongoji, pamoja
na taasisi zao ilikuleta maendeleo endelevu ikiwa pamoja na kuwashawishi wananchi
kushiriki katika michakato ya maendeleo na kuchochea ufanisi na utendaji wa serikali
za mitaa.
Mwezeshajihuyo,
BW.SAMUEL STANLEY amesema mradi huo unategemea uwajibikaji kutoka pande zote mbili,yaani
wananchi na viongozi wao ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya maendeleo katika halmashauri zetu za Kibaha.
Mmoja wa washiriki
wa mafunzo hayo ambayo pia yamewapatia elimu ya kodi, BW.HENRY MAKUNGU katika kuhakikisha
uwajibikaji katika sekta ya umma,kuzingatia haki za msingi za wananchi wa kawaida
badala ya kuwapendelea wananchi na wawekezaji matajiri tu.
BW.MAKUNGU ametoa mfano wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu
linapokuja suala zima la ulipaji kodi, ambapo mfanyabiashara mkubwa anapewa msamaha
wa kodi wa miaka 5, wakati wajasiriamali wadogo wa nchini anaanza kudaiwa kodi siku
ya kwanza anapoanza biashara na vinginevyo, wakusanya kodi wanaweka makufuli yao
siku hiyo hiyo, hivyo amependekeza serikali kuangalia upya utaratibu huo kwa kutoa
kipindi cha miaka sawa na hiyo kwa wajasiriamali wadogo wanapoanzisha biashara katika
suala zima la kujikimu kimaisha.
END
Comments
Post a Comment