VIDEO-WANAWAKE WAGWAYA KUGOMBEA MAJIMBONI WAKIMBILIA VITI MAALUM.
Ben
Komba/Pwani-Kibaha/7/24/2015 12:02:11 PM
Hali ya
wanawake kuwa nyuma katika kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi
imejitokeza kwa kiasi kikubwa katika mchakato wa kuwatafuta wagombea ambao
watawakilisha vyama vyao katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25 mwaka huu.
Kati ya
wagombea wa nafasi ya udiwani kata ya Tumbi mjini Kibaha, Angalau mwanamama
NURU MSADALA MAGEGE ameamua kujitokeza kupambana kuhakikisha ile asilimia
hamsini kwa hamsini ya uwakilishi inafikiwa.
BIBI.NURU
MSADALA MAGEGE ambaye alikuwa kivutio kwa wana ccm ambao wamehudhuria mkutano
huo, kwa kuweza kujieleza kwa ufasaha akiwa ni mwanamke pekee kati ya wagombea
wanane ambao wote ni wanaume.
Amewaahidi wana
CCM ambao wamehudhuria mkutano huo wa kampeni za ndani kwa ndani za chama katika
Kata ya Tumbi, Tarafa ya Kibaha mjini Kibaha kuwa atahakikisha anasimamia
majukumu yake ya kuwakilisha wananchi kwa uaminifu mkubwa ili kuweza kuwaletea
maendeleo endelevu wananchi.
Mbali ya
kujitokeza mwanamama huyo, Upande wa vijana napo kuna ambao wamejitokeza
mmojawapo akiwa mwanafunzi wa Chuo Cha
Bandari, BW.HEMED CHANYIKA ambaye yeye kwa upande wake amesema kuwa sasa
umefika wakati kwa vijana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili wapate watu
wa kuwasemea katika vyombo vya kutoa maamuzi.
END.
Comments
Post a Comment