WAKAZI KISARAWE WALALAMIKIA KUPORWA ARDHI NA WAVAMIZI WANAOSHIRIKIANA NA VIONGOZI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/7/9/2015 1:19:31 PM
Wananchi wa mtaa
wa Kiluvya A,kata ya Kiluvya tarafa ya Sungwi wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani
wametaka vyombo vinavyohusika na utoaji haki wa kisheria kushugulikia mgogoro
wa ardhi yenye ukubwa wa heka 338 walizoporwa na wanaodaiwa wawekezaji.
Mmoja wa
wakazi wa Kiluvya, BW.ABUBAKAR YUSSUPH amesema kama wamiliki wa maeneo
yaliyovamiwa ambao mpaka sasa wamekuwa wakizungushwa pamoja na suala hilo
kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.
BW.YUSSUPH
ameeleza kutoridhishwa na mwenendo wa kesi ya kuporwa ardhi na uongozi wa
kijiji na kupewa mabepari, kwa njia ya kughushi nyaraka na kilio cha kikubwa ni
Polisi kuchelewesha kupeleka vielelezo kwa mwendesha Mashtaka wa serikali kanda
ya Pwani.
BW.YUSSUPH
amefafanua kuwa kesi hiyo imedhoofishwa kwa makusudi ili kutoa fursa kwa
wavamizi kuchukua eneo hilo ambao idadi yao ni 15 na wanababaisha watu 250 na
mamlaka husika zinajua kuhusiana na hilo.
Naye mkazi
wa Mtaa wa Kiluvya, BIBI.ALFREDINA RAPHAEL amesema yeye amekaa eneo hilo toka
mwaka 1972, Lakini kumejitokeza watu ambao wanadai kuwa eneo hilo ni lao na
walikuwa wanaharakati ya kutaka kumiliki eneo hilo kutokana tu wao wana fedha.
BIBI.RAPHAEL
ameshangazwa na serikali na CCM ambao wanajua kinaga ubaga kuhusu nani ana haki
ya kumiliki eneo hilo, lakini kutokana na rushwa viongozi wamekuwa wakifumbia
macho mgogoro huo.
BIBI.RAPHAEL ameongeza kuwa mpaka sasa hatima
yao haijulikani hasa kwa viongozi wao ambao wamewateua kufuatailia suala hilo
ili kufahamu ukweli wa ambao upo bayana, ingawa wavamizi kwa kushirikiana na
viongozi wanataka kupotosha ukweli.
Nilipata
bahati ya kuongea Mmoja wa wanaolalamikiwa kati ya watu 15 wanaodaiwa kuvamia
eneo hilo kinyume cha taratibu, BW.ZEDI ABDUL ambaye kwa upande wake amesema
kuwa eneo hilo wamelinunua kutoka kwa BW.SAID BAKARI MAZOEA.
BW.ABDUL amesema yeye na wenzie wakiwa wamejipanga kwa
ajili ya kuanza upimaji ndipo wananchi walipojitokeza na kuzuia zoezi hilo,
hali ambayo limewasababishia hasara kubwa.
END.
Comments
Post a Comment