VIDEO-MWENYEKITI WA UVCCM KIBAHA MJINI AJITOSA KIBAHA MJINI.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/7/10/2015 7:14:19 AM
Katika hatua inayoashiria kuwa uchaguzi wa mwaka huu utatawaliwa na wagombea vijana kutokana  na watu wa rika hilo kuzindukana kutoka katika usingizi mzito na kuamua kushiriki siasa kikamilifu.

Mara hii Mwenyekiti wa UVCCM halmashauri ya mji wa Kibaha, BW.IDD KANYALU ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi hiyo kupitia chama hicho katika kata ya Kongowe ambayo nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na BW.SLUM BAGMESH.

BW.KANYALU akitangaza nia amewaahidi wananchi wa Kata ya Kongowe iwapo atabahatika kuteuliwa na chama chake kugombea udiwani katika kata hiyo, atashirikiana nao kwa hali na mali kuboresha hali ya mambo.


END. 

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA