VIDEO-MAGAIDI WASAMBARATISHWA PWANI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/7/21/2015 12:24:57 PM
Jeshi la
Polisi mkoani Pwani limewakamata wahalifu 25 na silaha mbalimbali ambazo
zinasadikiwa kufanya vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali nchini.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Pwani Mrakibu mwandamizi msaidizi wa Polisi,JAAFAR IBRAHIM
akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Kibaha amesema mafanikio
hayo yamefuatia operesheni maalum inayoendelea mkoani hapa.
Kamanda
JAAFAR amefafanua kuwa operesheni
imefanyika kati ya Juni 20 mpaka Julai 20, ambapo katika kipindi hicho silaha
ya SMG no.14302621,risasi 30 za SMG ndani ya magazine,visu 11,mapanga 4,
majambia 3,risasi 20 za SMG, risasi 103
za shortgun, Bomu la kienyeji 3,vipande vidogo vya nondo 42, fyuzi
zilizotegwa 24 na fyuzi zilizo tupu 56.
Kamanda
JAAFAR amefafanua kuwa mafanikio hayo yamepatikana kufuatia ushirikiano mkubwa
kutoka kwa jamii na kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwakamata wahalifu hao.
END
Comments
Post a Comment