VIDEO-WAJASIRIAMALI WA NDANI WAATAMIWE VYEMA ILI KULETA MAENDELEO.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/3-7-2015
Wananchi wametakiwa kuwa makini katika kuhakikisha nchi inafikia malengo ya maendeleo endelevu ili kujikwamua na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazowakabili hususan ya kiuchumi.

Mwezeshaji kutoka shirika lisilo la kiserikali la -YPC-YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE ambalo limeandaa semina hiyo kwa kushirikiana na ACTION AID , BW.SAMUEL STANLEY amesema lengo la Semina hiyo ni kuutambulisha mradi wa ViVA yaani sauti za vijana kwenye uwajibikaji.

BW.STANLEY amesema kupitia mradi huo wanategemea kuwajengea uwezo vijana na wananchi kwa ujumla kutambua nafasi yao katika kuchoche uwajibikaji katika vijiji na vitongoji, pamoja na taasisi zao ilikuleta maendeleo endelevu ikiwa pamoja na kuwashawishi wananchi kushiriki katika michakato ya maendeleo na kuchochea ufanisi na utendaji wa serikali za mitaa.

Mwezeshajihuyo, BW.SAMUEL STANLEY amesema mradi huo unategemea uwajibikaji kutoka pande zote mbili,yaani wananchi na viongozi wao ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri zetu za Kibaha.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambayo pia yamewapatia elimu ya kodi, BW.HENRY MAKUNGU katika kuhakikisha uwajibikaji katika sekta ya umma,kuzingatia haki za msingi za wananchi wa kawaida badala ya kuwapendelea wananchi na wawekezaji matajiri tu.

BW.MAKUNGU  ametoa mfano wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu linapokuja suala zima la ulipaji kodi, ambapo mfanyabiashara mkubwa anapewa msamaha wa kodi wa miaka 5, wakati wajasiriamali wadogo wa nchini anaanza kudaiwa kodi siku ya kwanza anapoanza biashara na vinginevyo, wakusanya kodi wanaweka makufuli yao siku hiyo hiyo, hivyo amependekeza serikali kuangalia upya utaratibu huo kwa kutoa kipindi cha miaka sawa na hiyo kwa wajasiriamali wadogo wanapoanzisha biashara katika suala zima la kujikimu kimaisha.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA