MNEC ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE KIBAHA MJINI.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/7/15/2015 11:19:52 AM

Mjumbe Wa Halmashauri Kuu Ya Taifa Ya chama cha Mapinduzi kutoka Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW.RUGEMALIRA RUTATINA ametangaza rasmi kuwania kiti hicho cha ubunge ikiwa ni katika suala zima la kuwaletea wana Kibaha maendeleo.

Akitangaza nia hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Kibaha katika tukio nadra sana kuvuta watu kutoka maeneo mbalimbali ya mji huu, BW.RUTATINA amesema kuwa yeye hana fedha za kugawa kama njugu lakini anazo mbinu za kumkomboa mwananchi wa kawaida kutoka katika lindi la umaskini.

BW.RUTATINA amewataka Watanzania hususan wakazi wa Kibaha kutokubali kununuliwa kwa jinsi yoyote ile ili kuepuka kuwekwa mfukoni mwa watu kwa kupewa shilingi 50000 kwa ajili ya kumchagua mtu kwa miaka mitano ya uwakilishi.

Mbunge huyo hakusita kuelezea shukrani zake kwa wananchi kutokana na kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia akitangaza nia pamoja na juhudi mbalimbali zilizofanywa na baadhi ya watu katika chama kuzuia viongozi wa Kata na matawi kukatazwa kufika katika tukio hilo.

END.


Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA