MKUU WA MKOA WA PWANI AZINDUA VIATAMBULISHO VYA URAIA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/30/6/2014 Mkuu wa mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA amepongezea hatua ya serikali ya kutoa vitambulisho vya uraia ili kuweza kutambua wageni na raia halali wa nchi hii ya Tanzania. Akizungumza katika kipindi cha uzinduzi wa usajili wa watu mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amesema jukumu hilo linaloratibiwa na NIDA ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi na ni maelekezo ya serikali ya awamu ya nne. Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amewasisitiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha jukumu hilo linatekelezeka kama serikali ilivyoaagiza, kwa kuipa NIDA ushirikiano wa hali na mali ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa vitambulisho vya uraia. Ameagiza iwapo kutakuwa na tatizo lolote amewataka watendaji kumpa taarifa katika kipindi mwafaka, ili kuepuka kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa letu. Awali akizungumza kukmaribisha Mkuu wa mkoa wa Pwani,...