NHIF COAST.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/12:19/17-06-2013
Mfuko wa
Bima ya afya Taifa una mpango wa kuhakikisha unashughulikia kero zote
zinazowakabili wanachama wake zinashughulikiwa ili kufikia malengo ambayo
imejiwekea wa kutoa huduma sthahili kwa wanachama wa mfuko huo.
Mkurugenzi
mtendaji wa mfuko wa Bima ya afya wa Taifa, BW. EMMANUEL HUMBA ameyaongea hayo
katika kikao maalum kilichowakutanisha wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa
mkoa wa Pwani.
BW.HUMBA
amesema kwa kuanzia watapeleka madaktari bingwa kwa ajili ya wilaya ya Mafia
ili kuweza kwenda kutoa huduma kwa wanachama wao wanaosihi na kufanya kazi
wilayani humo kutokana na wanachama wao kukabiliwa na tatizo la usafiri wa
uhakika.
BW. HUMBA
amefafanua kuwa kwa wanachama wa mfuko huo wanaosihi Mafia gharama zote za
huduma watakazopatiwa zitabebwa na mfuko wa Bima ya afya, wakati wananchi wa
kawaida itawalazimu kulipia uchangiaji wa huduma ya afya kama ilivyopangwa na
halmashauri au mkoa.
Ameongeza
madaktari bingwa hao watakuwa katika vituo viwili cha Mafia na katika hospitali
maalum ya rufaa ya mkoa, kwa mpango huo madaktari bingwa hao watatolewa
Muhimbili, kwa kutambua mahitaji ya wananchi ya kukutana na madaktari bingwa
kutokana na kukabiliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.
Naye mkuu wa
mkoa wa Pwani, BIBI.MWANTUMU MAHIZA amesema mfuko wa afya umekuwa kimbilio kubwa kwa wananchi
ambao kwa muda mrefu walikuwa hawana njia nyingine za kupata matibabu.
BIBI.MAHIZA
ameongeza kwa sasa wananchi wa mkoa wa Pwani wamehamasika vya kutosha kuhusiana
na huduma zinazotolewa na mfuko huo kwani umewaepushia wananchi kuuza mali zao
wanapokabiliwa na matatizo ya kiafya ili kujitibu.
Aidha
amewashukuru watu wa Bima ya afya kuuipatia hospitali ya msaada wa zaidi ya
shilingi milioni 300, ikiwa pamoja na kuelekeza kununuliwa kwa chombo cha
kupima damu salama ili kuweza kuboresha huduma hiyo katika mkoa wa Pwani.
END.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/18-06-2013
Katika hali
ya kushangaza Baba mmoja anayekwenda kwa jina la IGNASIUS KAIHURA ameikana
familia yake ya watoto wane na kudai kuwa hawatambui kutokana na sababua ambazo
hazipo bayana.
Mwandishi wa
habari hizi ameshuhudia watoto wane wakiwa na Mama yao BIBI. LUCY KAIHURA akiwa
na watoto wake ambao wametelekezwa na aliyekuwa mume wake ambaye ni mhandisi wa
mitambo katika Jeshi la wananchi waTanzania.
BIB I.
KAIHURA amebainisha kuwa yeye alikutana na BW.INFGASIUS wakati akiwa mwanafunzi
katika chuo kikuu cha Dar es Saalam na kufunga ndoa ambayo iliwawezesha kupata
watoto hao wanne.
BIBI KAIHURA
amebainisha kuwa siku moja alikwenda ofisi kwa mume wake kufuata mahitaji ya
familia na kujitambulisha ndipo alipoambiwa kuwa BW.IGNASIUS KAIHURA
amejiandikisha Jeshini kama yupo mwenyewe na hana familia inayomtegemea kitu
ambacho sio kweli zaidi sikiliza kilio cha mama huyu akiwa na watoto wake ambao
ameachiwa.
END

Comments
Post a Comment