SIASA YAWAKWAMISHA WADAU WA MAENDELEO

Ben Komba/Pwani-Tanzania

Suala la wananchi kusaidiana na serikali katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo imeingiliwa na sintofahamu kutokana na baadhi ya wawakilishi wa wananchi kuwa na mawazo potofu kuhusiana na misaada inayotolewa na wadau wa maendeleo wa maeneo yao na nje.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia kujitokeza kwa hali hiyo kayika Kata ya Ubena, ambapo mwananchi mfugaji wa Kimang’ati, BW.ALMAS MGUSA aliyetoa msaada wa mbao, misumari na mifuko ya udongo ulaya kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa baadhi ya majengo muhimu katika shule ya Msingi Tukamisasa.

Akitoa msaada huo, BW.MGUSA amesema yeye ametoa msaada huo kwa ajili ya kuisaidia jamii ya hapo na hasa ikizingatiwa kuwa yeye mwenye ni mkazi wa muda mrefu wa eneo hilo la Ubena wilaya ya Bagamoyo.

Amesema hatua hiyo ya kutoa misaada kwa shule ya msingi Tukamisasa inafuatia ombi la mwenyekiti wake wa kijiji wa kuomba msaada kutoka kwa wafadhili ili kukamilisha ujenzi wa darasa moja na amebainisha anafanya hivyo kwa lengo lka kuisaidia jamii na wala sio malengo ya kisiasa.

Naye mwenyekiti wa kamati ya shule ya Tukamisasa amemshukuru mwananchi huyo kwa msaada ambao ameutoa kwa shule yao na amewaaomba wafadhili wengine wajitokeze na hasa ikizingatiwa anachokifanya ni kwa faida ya jamii nzima.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA