SUMATRA WANYOOSHA MSTARI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/08/06/2013/13:32
Watanzania
wametakiwa kutoa ushirikiano stahili kwa SUMATRA wanapokuwa safarini ili kuweza
kupunguziwa kero zinazowapata wanapokuwa wanasafiri kuelekea maeneo mbalimbali
ya Tanzania.
Afisa mfawidhi
mkuu wa SUMATRA mkoa wa Pwani, BW.NASHON IROGA amesema hayo alipozungumza na
mwandishi wa habari hizi kufuatia uwepo wa kampeni maalumu ya ukaguzi wa mabasi
inayoendeshwa katika kituo kikuu cha mabasi mjini Kibaha.
BW.IROGA
amebainisha kuwa operesheni hiyo inayoendeshwa sambamba na askari wa usalama
barabarani, na lengo kubwa la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanadhibiti vitendo
vyote vya mabasi ya abiria kukatisha ruti,kutototoa tiketi kwa abiria na
mengine.
Amefafafanua
kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazojitokeza ambazo nyingi zinasababishwa na
madereva kukiuka taratibu za usafirishaji kwa makusudi kutokana na kuzongwa na tama,
akitoa mfano wa mabasi yanayofanya safari za Ubungo mpaka Mlandizi, ambayo
nyakati za jioni yanaishia Mbezi kutokana na abiria wa Mbezi kuwa tayari kulipa
nauli y ash.1000/= ambayo ni nauli ya Ubungo-Mailimoja.
Afisa huyo
mfawidhi wa SUMATRA mkoa wa Pwani, BW. NASHON IROGA ameongeza kuanzia sasa mtu
yoyote ambaye atakatisha ruti atachukuliwa hatua stahili za kisheria ikiwa
pamoja na kufuatiwa leseni na amewaasa wananchi kutokuwa na ghadhabu wakati wao
wanatekeleza wajibu wao.
END.
Comments
Post a Comment