RASIMU YA KATIBA NA MAPUNGUFU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/18-06-2013
Kuna mambo
ambayo yamejitokeza katika rasimu ya Katiba ilitolewa na Tume ya mabadiliko ya
Katiba, ambayo yasipotazamwa kwa umakini yanaweza kulisababishia Taifa vurugu
na kuhatarisha usalama wan chi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari wa habari hizi,
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE
lenye maskani yake mjini Kibaha ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa jukwaa la
katiba, BW.ISRAEL ILUNDE amesema kuna mapungufu takriban 50.
BW.ILUNDE
amesema katika rasimu hiyo ambayo imependwa na wananchi wa kada mbalimbali
ambayo kwa kiasi kikubwa imezingatia hisia za wananchi kwa kuweza kuyapa nafasi
masuala ambayo yalikuwa yamependekezwa na wananchi waliotoa maoni.
BW. ILUNDE
amefafanua kuwa kwa rasimu hiyo kutoa kipaumbele kwa suala la haki za binadamu
limeleta faraja kwa wananchi wengi hasa ikizingatiwa sehemu yenye kufuata
misingi ya haki za binadamu basi maendeleo lazima, kwani kutakuwa hakuna kundi
ambalo litakuwa linakandamizwa.
BW.ILUNDE
amebainisha tatizo ambalo linaweza kuleta sintofahamu baadaye ni suala la
serikali za Tanganyika na Zanzibar kujichagulia marafiki bila kutoa fursa kwa
serikali ya Muungano kuingilia kati na hivyo kutaufanya muungano wetu kuwa na
madoa madoa.
AIDHA
amesema kuna ibara 138 imekosekana katika rasimu ya katiba, ikiwa pamoja na
ibara ya 145 ambayo inalenga kutoa haki kwa makundi madogo ambayo
hayajafafanuliwa ni makundi ya aina gani.
END.
Comments
Post a Comment