AKINAMAMA WASAIDIWA MITAJI NA MKE WA MBUNGE KIBAHA MJINI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/11:59/14-06-2013
Wanawake katika kata ya Kibaha wameshauriwa kuhakikisha wanailinda amani ya nchi yetu kwa kutumia uwezo wao kuhakikisha kuwa amani na utulivu unadumu ili kuweza kupata maendeleo endelevu.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi mjini Kibaha, BI.MWATABU HUSSEIN amebainisha kuwa kinamama wao ndio wana jukumu la kuhakikisha wanasimamia heshima na maadili ya Taifa.
BI.HUSSEIN amesema amani ya Tanzania inapotezwa na watoto zao au waume zao kutokana na vitendo wanavyofanya ambavyo vinaweza kuhatarisha amani kwa kushauri au kukemea tabia zinazojitokeza katika ngazi ya awali, na watakao taabika yatakapotokea majanga ya vita ni kinamama, watoto na wazee.
Naye Mke Mbunge wa Kibaha mjini, BIBI SELINA KOKA ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kukutana wanawake ambao wamejiajiri katika sekta isiyo rasmi amesema amejiwekea utaratibu endelevu wa kuwafikia kinamama kila kata ili kuwaamsha wafanye shughuli za uzalishaji mali.
BIBI.KOKA katika mkutano huo alikabidhi hundi ya shilingi 18,000,00/= kwa ajili ya vikundi 6 vya kinamama wajasiriamali wa Kata ya Kibaha, sawa Kitambaa(jora moja) kwa ajili ya akinamama hao kupatiwa mafunzo ya utengenezaji batik ili waweze kujikwamua kutoka katika umaskini ili waweze kusaidia familia zao.
Amebainisha kuwa kuna masoko ya uhakika ya bidhaa zao, ambapo kwa sasa kinamama wanaojishughulisha na ukulima wa mbogamboga wamekuwa wakiuza bidhaa zao katika kampuni yake ya chakula ili kuongeza ari ya uzalishaji kwa kinamama.
END.
Comments
Post a Comment