WATENDAJI WAONYWA KUHUSU UZEMBE
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10:40/29-06-2013
Mkuu wa Mkoa
wa Pwani BIBI. MWANTUMU MAHIZA amewaonya watendaji katika halmashauri ya wilaya
ya Kibaha kufanya kazi kwa bidii na uwajibikaji kuepuka kuwajibishwa na
serikali.
Akizungumza
katika kikao maalum cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Kibaha,
BIBI.MAHIZA amebainisha kuwa wakati wa kuoneana aibu umepita na kila mtu
atawajibika kwa uzembe ambao ataufanya.
Mkuu wa mkoa
wa Pwani , BIBI.MAHIZA alianza kwa kuwaonya watendaji hususan wa ardhi ambao
wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha migogoro na wanapohamishwa wanaacha malumbano
ambayo hayana tija ambayo mengine yanatishia kusumbua hali ya amani na utulivu
uliopo.
BIBI.MAHIZA
ameelezea na kuchukizwa kwake na mgogoro unaoendelea katika kijiji cha Kisabi
ambapo maofisa ardhi kwa makusudi wamepima viwanja katika maeneo ya watu bila
kuwashirikisha wamiliki wa maeneo hayo, ambapo kuna maeneo yameuzwa kwa watu
zaidi ya sita, jambo ambalo amesema halikubaliki.
Kutokana na
kujitokeza kwa hali hiyo Mkuu wa mkoa wa Pwani ametoa siku 31 kwa wahusika
wampatie majibu sahihi kutokana na kadhia hiyo.
END.
Comments
Post a Comment