PWANI YAPANIA KUFUNGUA NDONDI,MAELFU WAFURIKA KUMUAGA MANGWEA,CCM YASIMAMISHA VIONGOZI BAGAMOYO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/06/06/2013/12:12
Mkoa wa
Pwani katika halmashauri ya mji wa Kibaha kumeanzishwa rasmi kampeni ya kuinua
mchezo wa ngumi ambao unaonekana kuwa na wapenzi wengi mjini na kubainika uwepo
wa vipaji wa mchezo huo kwa vijana wengi wa mjini hapa.
Kocha wa
mchezo huo anayetambuliwa na chama cha olimpiki ulimwenguni, BW. GAUDENCE UYAGA
amebainisha hayo baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi kando
ya Mazoezi ya mabondia anaowafundisha.
BW. UYAGA
amesema kuwa mchezo huo umekuwa hukikosa udhamini kutoka kwa wafadhili kutokana
na wengi kukosa msukumo wa kujua ni wapi wanaweza kupata wachezaji wa mchezo
huo, na kukatishwa tamaa na baadhi ya watu wanaojifanya mapromota ilihali
wakitanguliza mbele maslahi yao binafsi na kusahau haki za mabondia
wanaowachezesha.
BW.UYAGA
ametoa mfano kuwa kuandaa pambano moja la ngumi , Bondia inampasa kukaa kambini
si chini ya miezi mitatu na katika muda
huo bondia anahitajika kutumia si chini ya shilingi laki 6, ambapo utakuta
bondia analipwa ujira kati ya shilingi 350,000 mpaka 400,000, ambazo
hazilingani na maandalizi ya kambi.
Nikiongea na
mmoja wa mabondia anaowapatia mafunzo katika Kitongoji cha Mlandizi katika
ukumbi wa SUPER NIGHT CLUB, ZUMBA KUKWE ametanabaisha kuwa yeye kwa upande wake
yupo vizuri na anaangalia mbele kupambana na mabondia kama THOMAS MASHALI,
FRANCIS CHEKA, MADA MAUGO na yeyote ambaye atajitokeza.
ZUMBA KUKWE
amesikitishwa na tabia ya mabondia wanaopangiwa kucheza yeyte kumkacha, na
kuwataka wajitokeze wapambane nae wasiogope.
END.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/6-6-2013/13:30
Mamia ya
watu jana walisimama kando kando ya barabara ya Morogoro kusubiri kushuhudia
mwili wa aliyekuwa mwanamuziki wa kizazi kipya Marehemu ALBERT MANGWEA katika
mji wa Kibaha bila mafanikio.
Wananchi hao
ambao walionyesha hamu ya kutaka kushuhudia mwili wa nguli huyo wa muziki wa
kizazi kipya ambaye alipatwa na mauti akiwa nchini Afrika Kusini na mwili wake
kuletrwa juzi, Jumanne.
Nimebahatika
kuongea na MADEE kutoka uwanja wa Jamhuri Morogoro,mwanamuziki wa kizazi kipya
ambaye amesema tukio la Msiba wa ALBERT MANGWEA
limetoa mwanga kwa jamii kuwa watu wanaowachukulia kuwa wao wanaofanya mziki ni wahuni kitu
ambacho tofauti na jamii inawakubali.
Nilitaka
kujua ni kitu gania ambacho kimemfanya kusema hivyo, ameweka wazi kujitokeza
kwa wananchi kwa wingi kwenda kumuaga Marehumu ALBERT MANGWEA, kiasi cha
kufanya uwanja huo kufurika pomoni na kufungwa milango, kitu kinachodhihirisha
heshima waliyonayo wanamuziki wa kizazi kipya katika jamii.
Naye mpasha
habari wangu aliyekuwa Morogoro ameongea kuwa ni vigumu kwa mtu aliye nje,
kuingia ndani ya uwanja kutokana na umati uliokuwepo kiwanjani hapo na huku
baadhi ya waombolezaji wakianguka kwa mstuko.
END.
Ben
Komba/Pwani –Tanzania/06-06-2013
Chama cha
Mapinduzi mkoa wa Pwani umesimamisha viongozi wa chama hicho katika wilaya ya
Bagamoyo kufuatia madai ya kuuza eneo
ambalo wanadai mali ya chama cha mapinduzi kwa mwekezaji.
Viongozi
waliosimamishwa ni pamoja na Katibu, mwenyekiti na mwenezi wa chama hicho cha
CCM wilaya ya Bagamoyo, kufuatia maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya CCM
mkoa wa Pwani.
Kutokana na
hali hiyo baadhi ya wadau wa chama hicho wamelalamikia hatua hiyo na kuiita ya
uonevu, toka CCM Bagamoyo haina hati za kumiliki eneo hilo na hivyo chama hicho
kukosa uhalali wa umiliki wa eneo hilo kama ilivyojidhihirisha katika hukumu
iliyotlewa na mahakama inayoruhusu mwekezaji huyo kuendelea na mipango yake ya
kuendeleza eneo hilo.
Nikiongea na
Katibu wa CCM katika mkoa wa Pwani, BIBI. SAUDA MPAMBALYOTO amesema kwa upande
wake yeye hawerzi kusema lolote toka maamuzi hayo yalitolewa kupitia vikao
maalum vya kichama hivyo kutokana na hali hiyo inakuwa vigumu kwake kuzungumza
lolote.
Na akashauri
kuwa iwapo kuna wanachama ambao hawakubaliani na hatua zilizochukuliwa na
wakiwa na vielelezo vya kutosha basi itakuwa vyema akaviwakilisha kwake kwa
ajili ya kuchukua hatua mwafaka kwa lengo zima la kuimarisha umoja na
mshikamano katika chama.
END.
Comments
Post a Comment