VIJANA WAJITOLEA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/08/06/2013/15:08
Katika hatua
inayoonyesha vijana sasa wanatambua majukumu na wajibu wao katika jamii,
wamejiunga na kuanzisha kikundi cha kujitolea katika kata ya Mailimoja mjini
Kibaha katika suala zima la kuboresha miundombinu katika eneo wanaloishi.
Mmoja wa
vijana ambaye nimeongea naye BW. IMANI CHANGAMOTO wakiwa katikati ya shughuli
hiyo ya kusawazisha miundombinu ya barabara ya maeneo yao ya kwa SHEKHE
MUDHIHIR kutokana na kuharibika vibaya katika kipindi cha mvua zilizopita.
BW.
CHANGAMOTO amebainisha kuwa kitu kikubwa ambacho kimewafanya wao kujitolea
kuziba mashimo maeneo yao ni kutokana na kujihadhari na dharura ambayo inaweza
kujitokeza, hususan kuugua ghafla na majanga mengine ya asili ambayo yanatokea
bila taarifa ilihali miundombinu ikiwa mibovu.
Naye
Mwenyekiti wa Kikundi hicho cha NYOTA NJEMA, BW. MANSOOR LIPAMBILA amesema eneo
ambalo lilikuwa korofi zaidi ni karibu ya hospitali ambako kulikuwepo na
mahandaki ambayo yalikuwa inawapa wakati mgumu madereva ambao wanatumia
barabara hiyo kwenda na kurudi maeneo mbalimbali.
BW.LIPAMBILA amewataka wananchi hususani vijana kuwa na
moyo wa kujitolea ili maeneo yanayowazunguka yasiwe na kero ambazo zipo ndani
ya uwezo wao badala ya kutegemea kila kitu kufanyiwa na serikali kama
inavyojidhihirisha katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, na kutoa mfano mbwa
anaweza kugongwa eneo Fulani lakini hamna mtu atakayejitokeza kuchukua mzoga
huo kwenda kuufukia na matokeo yake hali hewa kubadilika ingawa kulikuwa na
uwezo wa kumfukia mzoga huo.
END.
Comments
Post a Comment