Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013/10:03 Chama cha marefa wilayani Kibaha kinaendesha program maalum ya mafunzo kwa marefa wapya wenye kutaka kujiendeleza kuwa waamuzi katika ngazi mbalimbali za ligi za mchezo huo. Katibu wa Chama cha marefa wilayani Kibaha ambaye pia ndio refa bora wa ligi ya VODACOM msimu uliopita BW.SIMON MBELWA amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha kuzalisha marefa wapya. BW.MBELWA amefafanua kuwa katika mambo ambayo yatazingatiwa katika mafunzo hayo ni ufundishaji wa sheria 17 za soka ambazo kila mwamuzi anapaswa kuzifahamu kwa ufasaha ili kuepusha malalamiko na wakati mwingine hata vurugu katika mchezo huo. Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, BW. GEORGE amesema kwa kupatiwa mafunzo hayo kutawasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi wakati wakichezesha mechi za michuano mbalimbali. END.
Ben Komba/Pwani=Tanzania/11:56 Umoja wa Wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni na mahoteli UGEHOKI mjini Kibaha wameilalamikia halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kuendelea kutoza kodi ambayo imefutwa kisheria. Katibu wa UGEHOKI, BW.RICHARD NGELEJA amesema hayo katika mkutano wa wanachama wa umoja huo uliofanyika katika ukumbi wa COUNTRYSIDE,Ambapo amenukuu majadliano ya kikao cha nane cha bunge cha tarehe 22 juni 2012. BW.NGELEJA amebainisha kuwa katika kikao hicho cha bunge ambacho kilijadili kuhusu ushuru wa hotel levy ipunguzwe kutoka 20% hadi 18% au 16%,na serikali inakamilisha zoezi lakuhuisha sheria ya utalii ya mwaka 2008 iliyoanza kutumika mwezi Julai,2009. Naye Mwenyekiti wa UGEHOKI, BW.FABIAN MAJAGA amebainisha kuwa wao wana vielelezo vyote vinavyoonyesha kufutwa kwa ushuru huo wa nyumba za wageni na mahoteli ikiwa pamoja hansard ya Bunge ambayo inaeleza wazi kufutwa kwa ushuru huo. BW.MAJAGA ameongeza kuwa hatua mbali mbali wamechukua ikiwa ...
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/07/2012/16:32:18 FIRE SOCIAL CLUB ya mijini Kibaha imefanya kikao chake cha uchaguzi mkuu na kufanikiwa kupata viongozi watakaoiongoza kwa kipindi cha miaka mitatu, ambapo uongozi huo umenuia kufanya mambo mabalimbali katika kuhakikisha michezo inakuwa ajira ya kutegemewa na vijana. Katika uchaguzi huo Mwenyekiti amechagulia kuwa JUMA MBWANA, na nafasi ya Katibu ikichukuliwa na RICH KIBAJA, Mweka hazina akiwa KESSY PONSI na mtunza vifaa akichaguliwa kuwa ni MESHAKI KAIRA. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa FIRE SOCIAL CLUB, RICH KIBAJA amebainisha kuwa lengo ni kukuza michezo hususan timu ya soka ambayo tayari ipo, kwa kuibua vipaji vya vijana ambao wanahitaji usaidizi mdogo ili waweze kusonga mbele katika medani ya michezo. KIBAJA ameongeza kuwa michezo ina umuhimu mkubwa kwa binadamu toka michezo ni starehe, afya na burudani. END
Comments
Post a Comment