WALIMU WAHIMIZWA KUCHAPA KAZI KWA BIDII NEEMA YAJA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/29/07/2016 17:53:55
Mkuu wa wilaya ya Kibaha amewataka Walimu wakuu wa shule za Msingi wilaya ya Kibaha kufanya kazi kwa uadilifu katika kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda wilaya hapa.

Mkuu wa wilaya Kibaha BIBI. ASSUMPTER MSHAMA ameyazungumza hayo alipokutana na Walimu wakuu kutoka shule za Msingi wilayani Kibaha pamoja na mambo mengine kuzungumzia maendeleo ya elimu.

BIBI. MSHAMA ameelezea kusikitishwa kwake na kuporomoka kwa kiwango kutoka nafasi ya nne kitaifa hadi kufikia nafasi ya tisa kurudi chini na kuwataka wamueleze wamekwama wapi ili aweze kuwakwamua na kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Hivyo amewasisitiza walimu wakuu kuchukua hatua kwa walimu wote wanaokwenda na kinyume na utaratibu wa kazi ili kuinua kiwango cha maendeleo ya elimu ili ikiwezekana turudie nafasi ya nne au ya kwanza kabisa.

Mwalimu UHAI KAMBI LEGEZA amemuomba Mkuu wa wilaya Kibaha kuhakikisha uimarishaji wa miundombinu ya elimu iende sambamba na ujenzi wa ofisi za walimu ambazo nyingi hazina hadhi anayostahili Mwalimu.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA