TALGWU WACHAGUANA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/08/07/2016 10:05:19
Chama cha
wafanyakazi wa serikali za mitaa katika Mkoa wa Pwani wamechaguana kupata
uongozi utakaouongoza katika kipindi kijacho.
Akitangaza matokeo
ya uchaguzi huo,Kaimu Mwenyekiti wa
Taifa wa TALGWU, BW. SELEMANI KIKINGO amewataka wanachama hao kuongeza
mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
BW. KIKINGO
ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutawezesha chama chao kupata mafanikio
wanayotarajia katika kusimamia maslahi na haki za wafanyakazi wa serikali za
mitaa.
Mbali ya
viongozi wengi kuchaguliwa kutoka makundi mbalimbali, Chama hicho kimefanikiwa
kupata Mwenyekiti mpya wa Mkoa, BW.OBADIA MWAKASITU na BW. KULWA MASAMBU akichaguliwa kuwa mjumbe kamati ya utendaji
Taifa na BW. MASAU MASAU akichaguliwa kuwa mjumbe baraza kuu TALGWU Taifa.
Akiuzungumza mara baada ya kuchaguliwa, Mwenyekiti mpya wa TALGWU Mkoa wa Pwani amewashukuru wanachama wote kwa kumchagua na kuwataka kuvunja kambi ili washirikiane kukijenga chama hicho cha wafanyakazi wa serikali za mitaa mkoani hapa.
END
Comments
Post a Comment