MWAROBAINI WAPATIKA ENEO LA SOKO KIBAHA

 Ben Komba/Pwani-Tanzania/21/07/2016 12:39:22

Mkuu mpya wa wilaya ya Kibaha, BI.ASSUMPTA MSHAMA amepata mwarobaini wa tatizo la soko mjini Kibaha kwa kufanya ziara eneo linalotarajiwa kujengwa soko akiambatana na wafanyabiashara na watendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha.

Mkuu wa wilaya MSHAMA amesema kuwa halmashauri ina wajibu wa kuonyesha eneo la soko ili wafanyabiashara wenye uwezo  wa kujenga wafanye hivyo na kuondoa sintofahamu iliyopo kufuatia soko la zamani kuwa karibu na barabara na hivyo kuhitajika kubomolewa kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro.

BI.MSHAMA kwa kufanya hivyo amefanikiwa kwa kiasi Fulani kutatua mgogoro uliokuwepo kati ya halmashauri na wafanyabiashara ambao walikuwa wanahitaji kufahamu iwapo soko hilo lingevunjwa hatma yao itakuwaje.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Kibaha MSHAMA amesikitishwa na kitendo cha halmashauri ya mji kuvunja nyumba za wananchi kwa notisi ya siku saba na bila kuzingatia iwapo nyumba hizo zipo kwa takriban miaka 30 na huku kukiwa na familia zenye watoto na wazee.

Naye ajuza DOGA HASSAN mwenye umri wa miaka zaidi ya 90 hakusita kutoa machozi kufuatia kuvunjwa kwa nyumba yake ambayo ameishi kwa kipindi cha miaka 30 na kupata watoto na wajukuu akiwa eneo hilo ambalo kwa sasa ameondolewa kwa nguvu na kumfanya ashindwe kujua hatma ya maisha yake.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA