VIDEO-MWAROBAINI WA SOKO WAPATIKANA KIBAHA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/21/07/2016 12:39:22
Mkuu mpya wa
wilaya ya Kibaha, BI.ASSUMPTA MSHAMA amepata mwarobaini wa tatizo la soko mjini
Kibaha kwa kufanya ziara eneo linalotarajiwa kujengwa soko akiambatana na
wafanyabiashara na watendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha.
Mkuu wa
wilaya MSHAMA amesema kuwa halmashauri ina wajibu wa kuonyesha eneo la soko ili
wafanyabiashara wenye uwezo wa kujenga
wafanye hivyo na kuondoa sintofahamu iliyopo kufuatia soko la zamani kuwa
karibu na barabara na hivyo kuhitajika kubomolewa kupisha upanuzi wa barabara
ya Morogoro.
BI.MSHAMA
kwa kufanya hivyo amefanikiwa kwa kiasi Fulani kutatua mgogoro uliokuwepo kati
ya halmashauri na wafanyabiashara ambao walikuwa wanahitaji kufahamu iwapo soko
hilo lingevunjwa hatma yao itakuwaje.
Aidha Mkuu
wa wilaya ya Kibaha MSHAMA amesikitishwa na kitendo cha halmashauri ya mji
kuvunja nyumba za wananchi kwa notisi ya siku saba na bila kuzingatia iwapo
nyumba hizo zipo kwa takriban miaka 30 na huku kukiwa na familia zenye watoto
na wazee.
Naye ajuza
DOGA HASSAN mwenye umri wa miaka zaidi ya 90 hakusita kutoa machozi kufuatia
kuvunjwa kwa nyumba yake ambayo ameishi kwa kipindi cha miaka 30 na kupata
watoto na wajukuu akiwa eneo hilo ambalo kwa sasa ameondolewa kwa nguvu na
kumfanya ashindwe kujua hatma ya maisha yake.
END
Comments
Post a Comment