MIFUGO TATIZO KITONGA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/07/2016 08:57:26
Hali ya sintofahamu imeibuka katika kijiji cha Kitonga kata ya  Vigwaza wilaya mpya ya Chalinze kufuatia wafugaji kuingiza ng’ombe mashambani mwa wakulima na kuharibu mazao yao.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kitonga BW. LAMBERT MSAWANGA amesema kuwa hali ni mbaya kijijini hapo kiasi cha kutishia amani na usalama kutokana na wafugaji kuingiza mara kwa mara mifugo yao katika mashamba ya wakulima.

BW. MSAWANGA ameongeza kuwa mara zote anapojaribu kutatua suala hilo imekuwa nggumu kutokana na dharau na ubabe unaoonyeshwa na baadhi ya wafugaji na hivyo jamii kuishi na wasiwasi.

Naye mwananchi BW.SEIF ABDALLA  MPEMBENWEambaye shamba lake lilivamiwa na ng’o mbe wapatao 30 na kuharibu eka moja na nusu za mpunga na hivyo kurudisha nyuma jitihada zake za kuweka akiba ya chakula iwapo angefanikiwa kuvuna.

BW.MPEMBENWE amebainisha mara zote wafugaji wanapoingiza ng’ombe mashambani unapowakuta wanatoa vitisho na iwapo ukimshataki unakamatwa wewe kama ilivyotokea kwa mjumbe mmoja wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ana kesi mahakama ya Lugoba maka sasa.

Hivi karibuni wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya, Mkuu wa mkoa wa Pwani, MHANDISI EVARIST NDIKILO amewaagiza wakuu wa wilaya kukabiliana na migogoro yote inayojitokeza sehemu yao badala ya kuiacha itatuliwe na mkuu wa mkoa.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA