VIDEO=BBC NA MCT WAWANOA WANAHABARI UCHAGUZI MKUU
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/15/2015 6:56:17 AM Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuhoji baadhi ya Habari mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambazo zinaweza kusababisha uvinjifu wa amani. Mwezeshaji katika mafunzo ya waandishi wa Habari ambayo yameandaliwa na BBC MEDIA ACTION kuhusiana na uandishi wa Habari wenye kufuata maadili katika kuripoti Habari za uchaguzi ambayo yamefanyika mjini Dar es Saalam, BW.ATTILIO TAGALILE amesema kuwa vyombo vya Habari vimekuwa vikiripoti kuhusiana na mambo ambayo yanaweza kusababisha vurugu. BW.TAGALILE ameongeza kuwa kauli kama Goli la mkono au nitachukua nchi mapema asubuhi kwa kauli kama hizo ambazo jamii inazipata kupitia vyombo vya Habari na kutozifanyia kazi ikiwa pamoja na Tume ya uchaguzi na waandishi wa Habari wenyewe kwani walikuwa na wajibu wa kufuatilia ili kupata ufafanuzi jinsi gani wanaweza kutekeleza goli la mkono na vipi itawezekana us...