VIDEO-WANANCHI BAGAMOYO WALALAMIKIA KUSITISHWA KWA MNADA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/26/2015 12:21:34 PM Wakazi wa kijiji cha Ruvu Darajani wilaya ya Bagamoyo katika mkoa wa Pwani wamelalamikia uongozi wa wilaya ya Bagamoyo ya kuzuia kufanyika mnanada katika eneo hilo kila siku. Mmoja wa wafanyabiashara wa ng’ombe ambaye nimebahatika kuongea naye,BW.DEOGRATIUS KIWALE amesema yeye kama mfanyabiashara wa ng’ombe wamekuwa wakinunua ng’ombe kutoka maeneo mengine na kuja kuwauza katika mnada huo wa Ruvu. BW.KIWALE ameongeza kuwa wao wamekuwa wakilipa kodi mbalimbali ambazo kwa njia moja au nyingine zimekuwa zimekuwa zinawasaidia wakazi wa kijiji hicho na kijiji chenyewe katika kuwawezesha kugharimia huduma mbalimbali za kijamii. Naye mkazi mwingine wa kijiji cha Ruvu,BW.SADALAH CHACHA amebainisha kuwa hatua ya kusimamisha mnada ni kuwakomoa wakazi wa Ruvu kutokana na wao kukataa kupokea wavamizi ambao wamevamia eneo hilo na Mkuu wa wilaya kuamrisha watu hao wapatiwe maeneo katika eneo lililovamiwa. BW.SADALAH amefafanua k...