HOTUBA YA MH.EDWARD NGOYAY LOWASSA KUTANGAZA NI YA URAIS
HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KWA AJILI YA KUTANGAZA NIA YA KUOMBA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KWA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTANGULIZI: Ndugu zangu wana-CCM na Watanzania wenzangu, Hii ni siku muhimu kwangu na kwa nchi yetu. Leo nimeamua kuwaita ili kuwatangazia rasmi Watanzania wenzangu azma yangu ya kutaka kuomba ridhaa ya chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), niweze kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nasema hii ni siku muhimu kwangu kwa sababu naamini historia yangu itainakili kama ni siku ambayo kwa mara ya pili katika maisha yangu nimejitokeza kuwania kuiongoza nchi yetu kupitia chama chetu. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini nilipojitokeza nikiwa pamoja na Rais Jakaya Kikwete; wakati ule sote tulikuwa wanasiasa vijana. Tulikwenda pamoja kuchukua fomu ndani ya Chama na baadaye tukafanya maz...