ZAHANATI YAPANULIWA MJINI KIBAHA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-3-2014:11:51
Zahanati
ya Mkoani inafanyiwa upanuzi kuwezesha kuchukua kinamama wajawazito
wapatao 250 mpaka 300 kwa mwezi na ujenzi huo unatarajia kutumia
shilingi Milioni 250
ikiwa ni mapato ya ndani ya halmashauri ya mji wa Kibaha.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa
Kibaha, BW.ISSA KANIKI amesema kuwa Zahanati ya Mkoani imekuwa na tatizo
kubwa linapokuja suala la kinamama wajawazito, ambapo kwa sasa Zahanati
ina vitanda vya kujifungulia kinamama wajawazito.
BW.KANIKI
ameongeza ujenzi huoo
utawanufaisha zaidi kinamama na watoto wachanga, Mpaka sasa mkandarasi
ameshapatikana na ujenzi unatarajia kukamilika Mei 30, moja ya majengo
yatakayojengwa ni holi la kupumzikia, holi la kinamama ambao
wamejifungua na wanaporudi nyumbani wanapata matatizo na kulazimika
kurudi hospitali.
aidha
amefafanua kuwa kila kitu kimekamilika na hakuna tatizo lolote na
mkandarasi yupo eneo la ujenzi akiendelea na kazi, ingawa ili upanuzi
ufanikiwe kunahitajika mchango wa hali na mali
kutoka halmashauri na maeneo mengine kwa wadau wa maendeleo wa sekta ya
afya.
Ujenzi
huo ambao unatarajiwa kuchukua kipindi cha miezi mitano kutoka Januari
mpaka Mei 30 mwaka huu, na kwa kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha
utoaji wa huduma kwa mama na mtoto katika kipindi hiki ambapo serikali
imevalia njuga kuboresha huduma za Baba,Mama na Mtoto.
Mwenyekiti
Chama cha Mapinduzi Kata ya Tumbi, BW.CHARLES KAPAMA ameipongeza
halmashauri ya mji wa Kibaha kusimamia na kutekeleza ilani ya uchaguzi
wa chama hicho katika kuhakikisha uboreshaji wa utoaji wa huduma ya
afya.
END.
Comments
Post a Comment