WAPONGEZA UTEKELEZAJI ILANI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/15-03-2014
Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara kuzunguka kila kata kuelezea mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kunakofanya na Rais DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE katika kipindi chake cha uongozi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Kibaha vijijini, BI.SIWEMA TUWA amesema kwa upande wao kama moja ya Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi wamejipanga kuunga mkono juhudi zilizofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa anavyotekeleza ilani ya uchaguzi wa chama hicho.

BI.SIWEMA amebainisha kwa kuanzia wameanza kufanya ziara yao katika kata ya Soga ambapo wamefungua matawi mawili ya wakereketwa, Ofisi ya Chama Kata na mradi wa kuku wa kufuga.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Kibaha vijijini, BW.HAMIS KANESA akijibu risala mbalimbali zilizosomwa kwake na Vikundi ambavyo amevikagua amesema Chama kimejipanga kusaidia wanajamii ambao wanajishughulisha na ujasiriamali.

BW.KANESA ameongeza kuwa kwa kuanzia atawasaidia vijana 48 wa BODABODA kwa kuwaletea taasisi ambayo inatoa mkopo wa Pikipiki aina ya BOXER ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Aidha BW. KANESA amewataka vijana ambao wamehitaji msaada wa kupatiwa mashine ya kufyatulia matofali katika kijiji cha Msufini na kiasi cha shilingi laki mbili, kwenda kuangalia thamani halisi ya mashine hiyo na kumjulisha kwa ajili hatua nyinginezo za kuwapatia msaada huo.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA