NISHATI MBADALA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/06-03-2014
Wananchi wilayani Kibaha wametakiwa kutumia nishati mbadala katika shughuli zao za kila siku ili kupunguza wimbi la uharibifu wa mazingira kama inavyojidhihirisha sasa.

Kaimu mkuu wa wilaya ya Kibaha, BI. HADIJA MRUMA akifungua uzinduzi wa kituo hicho cha kuzalisha mkaa bila kukata miti amesema kuanzishwa kwa mradi huo wa nishati mbadala na hatua muhimu katika kupunguza ukataji wa miti holela.

BI.MRUMA ameitaka jamii kuchangamkia teknolojia ya matumizi ya nishati mbadala ili kuweza kuleta mapinduzi ya misitu ambayo itasaidia kuokoa misitu yetu na uharibifu.

Akiongea katika uzinduzi wa Kituo cha kuzalisha mkaa mbadala bila kukata miti  kilichopo Mlandizi Msufini, Mkurugenzi wa TaTEDO, BW. ESTOMIH SAWE amesema kuna ongezeko kubwa la matumizi ya mkaa ambalo linatishia kusababisha jangwa.

BW.SAWE ameongeza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la ukataji miti kutokana na Jiji la Dar es Saalam kutegemea nishati ya mkaa ambao unatoka katika mkoa wa Pwani na hivyo siku zinavyozidi kwenda ongezeko la ukataji miti unazidi.

Amefafanua kuwa TaTEDO kwa kuliona hilo kwa na kushirikiana na Mjasiriamali BW.RAMADHAN SANZE ambaye alitoa eneo lake ili kuendesha mradi huo wa uzalishaji wa mkaa mbadala, ili kuweza kuokoa misitu kuangamia kutokana na ukataji miti holela.

BW.SAWE amewashukuru wadau mbalimbali kwa kutoa ushirikiano katika uendelezaji wa teknolojia hiyo ya nishati mbadala, wakiwemo UNDP, TFS, NEMC na wengineo wenye nia njema na suala la utunzaji wa mazingira.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA