RIDHIWAN ARUDISHA FOMU
Ben Komba/Pwani-Tanzania/927/13-3-215
Mjumbe wa NEC wa chama cha Mapinduzi BW.RIDHIWAN
KIKWETE ambaye pia ni mgombea wa ubunge wa Jimbo la uchaguzi Chalinze kupitia
tiketi ya Chama cha mapinduzi amerejesha fomu za kuwania nafasi hiyo.
Akipokea fomu hizo Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo,
BW.SAMWEL SALIANGA amesema mpaka sasa ofisi yake imeshapitia fomu ambazo
zimerajeshwa na kujiridhisha na mchakato unavyoendelea na hivyo kutoa fursa
rasmi kwa BW.KIKWETE kuanza kampeni muda wowote.
BW.SALIANGA amebainisha kuwa mpaka sasa vyama ambavyo
vimeshachukua fomu kugombea nafasi iliyo wazi Ubunge wa Jimbo hilo ambayo
imeachwa wazi kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, BW. SAID
MDOGO.
Amewataja vyama vitano ambavyo tayari vimechukua fomu
mbali ya CCM, ni CUF wamemsimamisha BW.ZAHOR PANDU, CHADEMA ni BW. MATHAYO
TOLONGEI na NRA mgombea wao ni BW.HASSAN ALMAS.
Akizungumza mara baada ya kurudisha fomu hizo, Mgombea
huyo wa CCM BW.RIDHIWAN KIKWETE amesema kuwa kati ya mambo ambayo atayatilia
kipaumbele ni kuwaunganisha wakulima na wafugaji.
BW.KIKWETE amebainisha kuwa itakuwa majanga makubwa
kwa yeye kuwabagua wakulima na wafugaji, toka MZEE KIKWETE akiwa CHIFU eneo hilo ndiye
aliwakaribisha wafugaji kuwa sehemu ya jamii ya Chalinze na kwa upande wake atachukua
fursa hiyo kuenzi yaliyofanywa na wahenga.
END
END.
Comments
Post a Comment