NYUKI NA FAIDA ZAKE.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/7/2014/10:00:49
Watanzania wameshauriwa kufuga nyuki wadogo ili waweze kujikomboa kiuchumi kutoka na asali ya nyuki hao kuwa na faida ya kiuchumi na kiafya kwa jamii.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la MATRIX lenye maskani yake mjini Kibaha, BW. MHEGELELE MDUDA amesema ufugaji wa nyuki hao ni muhimu kwa jamii kwani inasaidia kuongeza kipato kwa jamii na vilevile katika suala zima la uimarishaji afya.

BW.MDUDA ameongeza kuwa kufuga Nyuki wadogo ni rahisi kutokana na nyuki hao kutokuwa wakali na hivyo kutoweza kudhuru watu kulinganisha na nyuki wakubwa ambao wenyewe upenda kuweka maskani yao sehemu zenye utulivu.

Mkurugenzi huyo wa MATRIX, BW.MDUDA amefafanua kuwa nyuki hao ili waweze kuzalisha asali kwa wingi kinachotakiwa ni uwepo wa miti ya maua mbalimbali, kama milonge, Mastaferi na maua mbalimbali ya mwitu.

AIDHA amebainisha kuwa hali ya uwepo wa maji maji nayo ni muhimu kwa uzalishaji asali wa nyuki hao wadogo ambao wanapatikana na mizinga yao kwa mtu mwenye kuhitaji kufuga nyuki wadogo wa asali.

BW.MDUDA ameshauri Serikali kutupia macho na kuweka bajeti kubwa kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wa ufugaji wa Nyuki kuweza kupanua biashara zao ili waweze kujipatia kipato.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA