WANAWAKE KIBAHA WAJIANDAA KWA SHEREHE ZAO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/01-03-2014
Katika
kuadhimisha siku ya wanawake duniani, Jumuiya ya wanawake wa Chama cha
Mapinduzi mjini Kibaha, wametumia nafasi hiyo kutengeneza sare ya maadhimisho
hayo ikiwa ni njia ya kinamama wengine kujifunza kwa kutumia mbinu ya
ujasiriamali kujikwamua kiuchumi.
Kamera ya
mpiga picha iliwakuta kinamama hao nyuma ya ofisi za chama hico wilaya
wakitengeneza vitenge maalum kwa ajili ya siku ya kilele cha sherehe za
kinamama kwa ajili ya matumizi ya kushona mashati au kama kitenge kwa kinamama.
Comments
Post a Comment