MFUKO WA RAIS WA KUJITEGEMEA UMEBAKI JINA TU.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/1/5/2014 10:32:56 AM
Wanachama wa
mfuko Rais mjini Kibaha wamelalamikia hatua ya kusumbuliwa na watendaji wa
mfuko huo kutokana nakutopewa miko[po wanayohitaji pamoja na kulipa fedha za
akiba walizotakiwa kutoa kabla ya kupatiwa mkopo huo.
Mwandishi wa
habari hizi akiongea na mmoja wa mmoja wa wanakikundi wa kikundi cha Kiluvya B,
Mama EUNICE MACHA ambaye amebainisha kuwa kwa sasa ana takriban miaka
isiyopungua sita toka ametoa fedha za akiba kwa ajili ya kupatiwa mkopo huo,
lakini imekuwa wakizungushwa mpaka sasa.
Mama.MACHA
amebainisha kutokana na hali hiyo biashara zake zimekuwa zikiyumba na
kumsababishia maisha magumu na yasiyo na uhakika na akiwa hajui kama fedha zake
zikirudishwa zitakuwa na riba au la.
Mama.MACHA
ameongeza kuwa amekuwa mteja wa mfuko huo wa Rais kwa kipindi cha miaka 5, na
wameanza kudai amana zao toka mwaka 2008, lakini hakuna kilichofanyika
kuhusiana na malipo ya akiba za wanachama baada ya mfuko huo wa Rais kushindwa
kutimiza majukumu yake.
Naye BI.SARAH
KIMARO yeye akiwa mmoja wa wanachama wa
mfuko huo, amekuwa na wakati mgumu kuendesha maisha yake kutokana na kuwa fedha
zote alizokuwa anategemea zimeshikiliwa na mfuko huo.
Naye
BW.CHRISANT MVULA ameshangazwa na majanga yaliyoiukuta mfuko wa Rais wa
kujitegemea uliokuwa na dhima ya kuwasaidia wanachama wake kwa kuwapatia mikopo
kwa ajili ya kujikwamua na hali ngumu ya uchumi.
BW,MVULA
amebainisha kuwa kabla ya kuingia madarakani serikali ya awamu ya nne mfuko huo
ulikuwa ukifanya shughuli zake kwa weledi wa hali ya juu na kuweza kuwasaidia
kinamama katika masuala mbalimbali, lakini mara baada ya uongozi wa awamu ya
nne kuwa madarakani mfuko huo umekuwa ukipora wananchi wake badala ya
kuwasaidia.
Naye Meneja
wa mfuko wa Rais wa kujitegemea mjini Kibaha ambaye alikataa kutaja jina lake
amethibitisha kupokea malalamiko ya wanakikundi wa Kiluvya B, na amewataka
kufika ofisini kwake siku ya Januari 06 mwaka huu, ilikupeana ufafanuzi.
END.
Comments
Post a Comment