MCHELE BEI CHINI.



Ben Komba/PWANI-TANZANIA/1/2/2014 10:47:38 AM

Serikali nchini imetakiwa kujenga mazingira mazuri kwa wajasiriamali wazawa ili waweze kupambana na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na sheria ambazo hazizingatii mazingira ya halisi ya kiuchumi.

Mjasiriamali BW.OTTO KINYONYI mkazi wa Mlandizi wilayani Kibaha ambaye anamiliki kampuni ya KINYONYI INVESTMENT ambayo inashughulikia mazao ya nafaka katika soko la Mchele Mlandizi amesema sheria nyingi zinazotumgwa na serikali zimekuwa zinambana mjasiriamali.

BW.KINYONYI ametoa mfano wa mrundikano wa kodi mbalimbali ambazo mfanyabiashara anapaswa kulipa ambazo zinaambatana na makadirio batili, ongezeko la bei ya umeme ambayo itasababisha mlipuko wa bei ambao hivi karibuni  ulipoa, kutokana na gharama za uzalishaji kupanda.

Pamoja na changamoto hiyo BW. KINYONYI ameongeza pia kuna nyingine ikiwa pamoja na kukosekana kwa mvua za kutosha ambapo wakati mwingine inawabidi kuagiza mpunga kutoka Morogoro hasa inapotokea kuwepo kwa msimu mbaya.

BW.KINYONYI akizungumzia soko la mchele mwaka huu, amesema kuwa mchele umeshuka bei hadi kufikia kilo 1 shilingi 1050/=, na kutokana na hilo bei hiyo inakuwa katika masoko yote makuu ya mchele yaani Bonde la Mto Ruvu, Morogor na Mbeya.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA