BAJETI 2014/2015 WILAYA YA KIBAHA



Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-01-15/12:08

Halmashauri ya wilaya wilaya Kibaha katika mwaka wa fedha 2014 mpaka 2015 inatarajia kutumia shilingi 18,045,984,815/=  bila kuhusisha michango ya wananchi.

Hayo yamebainishwa na Ofisa mipango wilaya ya Kibaha, BW.ENOCK KIVELEGE wakati akiwasilisha makisio ya bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa halmashauri, BW.KIVELEGE amesema kati ya fedha hizo shilingi 15,713,153,623/= ni mchango toka serikali kuu.

BW.KIVELEGE ameongeza na fedha nyingine shilingi 2,332,831,192/= ikiwa ni mapato ya ndani ya halmashauri,na katika mwaka 2014 mpaka 2015 halmashauri ya wilaya ya Kibaha imekadiria kukusanya kiwango hico kikiwa ni mapato ya ndani.

BW. KIVELEGE ameongeza kuwa halmashauri imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni uhaba wa fedha wa kutekeleza shughuli zilizopangwa kufanyika, ufinyu wa mapato ya ndani na mchango wa wananchi kuwa mdogo kulinganisha na mahitaji ya halashauri.

Aidha, BW.KIVELEGE ameweka wazi malengo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015 ambayo ni kuimarisha vyanzo vya mapato na kuongeza ukusanyaji wa makusanyo ya ndani, kusimamia sheria, kuongeza tija katika kilimo,kuendeleza miundo mbinu, kujenga uwezo, kuhamasisha ushiriki wa jamii katika shughuli mbalimbali na kuhimiza ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi.

Awali akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kibaha, BW.CHRISTOPHER MDUMA amesema lengo la kuandaa kikao cha baraza la wafanyakazi halmashauri ya wilaya nikutoa nafasi kwa watumishi wa idara mbalimbali kupitia kwa karibu bajeti ya ya mwaka wa fedha 2014/2015 kwa lengo la kufanyia masahihisho kabla haijafikishwa katikakikao cha bajeti cha baraza la madiwani.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA