MWEKEZAJI ALALAMIKIWA

MWEKEZAJI AHARIBU MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/24-01-2014/10:15

Wakulima wa ushirika wa umwagiliaji Ruvu CHAURU wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani,wamelalamikia hatua ya mwekezaji wa Kichina katika shamba hilo kuvunja tuta linalozuia maji kufurika maeneo ya makazi wakati Mto Msua unapojaa.

Mmoja wa wakulima ambaye nimeongea naye,BW.SADALAH CHACHA amesema hatua ya kupasua ukingo wa kuzuia maji yasisambae maeneo ya makazi na kilimo inatishia usalama wa wakulima na mali zao kutokana tabia ya Mto Msua kufurika kipindi cha mvua za msimu na kuwa hatari kwa mustakabili wa shamba hilo.

BW. SADALAH amemwonyesha mwandishi wa habari hizi eneo maji yanaofikia wakati wa mafuriko ambapo yanajaa hadi kufiki futi 16 kutoka mkondo halisi wa maji na hivyo kuwepo na hatari ya kutokea mafuriko wakati wowote kutoka sasa.

Naye mkulima mwingine amebainisha kuwa tatizo la shamba hilo la ushirika ni kuendeshwa kibabe bila kushirikisha wananchi na hayo ndiyo matokeo yake, toka wakulima wa shamba hilo wengi wao ni wataalamu wa masuala mbalimbali kutokana na wengi wao kuwa watumishi wa umma na wafanyabiashara na wataalamu binafsi.

Kutokana na kuendeshwa kibabe kwa ushirika huo, Mbunge wa Bagamoyo BW.SHUKURU KAWAMBWA hivi karibuni alitembelea ushirika huo na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kutuma wakaguzi kufika shambani hapo kukagua akaunti ya maji ambayo wakulima wamechanga fedha zaoili waletewe maji.

Ushirika huo wenye wakulima wapatao 800 na eka karibu elfu 40 umekuwa ni tegemeo kwa wakulima kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Saalam, na ni moja ya meneo ambayo yanaweza kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula katika Mkoa wa Pwani.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA