MRAJIS ATANZUA MGOGORO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/1/9/2014 11:05:07 PM
Bodi ya
wajumbe wa Chama cha ushirika wa umwagiliaji-CHAURU- uliopo Bagamoyo mkoa wa
Pwani wamekosa sifa ya kuendelea kushikilia nafasi zao kutokana na kushindwa
kuwasilisha ukaguzi wa mahesabu kwa wakaguzi wa vyama vya ushirika nchini kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Akizungumza katika
Mkutano mkuu maalum wa ushirika huo, Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa
wa Pwani, BIBI.HADIJA MANG’ELA amesema taratibu za vyama vya ushirika zipo
wazi, iwapo hesabu hazijakaguliwa na mkaguzi wa nje kwa kipindi cha miaka mitatu
mfululizo bodi itapoteza uhalali.
BIBI.MANG’ELA
ameongeza kuwa mbali ya kupoteza hadhi ya kuwa wajumbe wa bodi, pia
watasimamishwa kugombea uongozi kwa kipindi cha miaka sita kama adhabu yao ya
kushindwa kutimiza majukumu yao basi sheria namba 48 kifungu kidogo cha 7 ya
sheria ya vyama vya ushirika itabidi kutumika.
Akijitetea mbele
ya mkutano huo maalum, Mwenyekiti wa Ushirika wa umwagiliaji CHAURU, BW.ZAHOR
SENG’ENGE amesema bodi la kuitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Matokeo makubwa
sasa, kwa nia ya kuhakikisha kila mwanachama anapata tija stahili.
BW.SENG’ENGE
amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2012 hesabu zao zimekaguliwa na
mkaguzi wa ndani na wanaangalia uwezekano wa kutafuta mkaguzi wan je ili na
afanye ukaguzi kama taratibu zinavyoelekeza.
Mwanachama BW.DAUD
KINDAMBA kwa upande wake alitaka mkutano huo maalumkuchukua hatua stahili dhidi
ya Bodi kama sheria kama Mrajis alivyobainisha katika mwongozo wa vyama vya
ushirika.
BW.KINDAMBA
amesema Mwenyekiti amekuwa akifanya vitu bila kuwashirikisha wanachama na ikiwa
pamoja na kutowasomea wanachama taarifa ya mapato na matumizi ya msimu uliopita
na badala yake yeye anakuja na bajeti ambayo mara zote imekuwa ikiongezeka na
kuwa mzigo kwa wakulima.
END.
Comments
Post a Comment