KWAYA YA MTAKATIFU DON BOSCHO YAFANYA HARAMBEE.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/29-01-2014/12:28
Jumla ya
shilingi Milioni tatu zimepatikana katika harambee ya kuiwezesha kwaya ya MTAKATIFU.DON
BOSCHO ya mjini Kibaha katika Mkoa wa Pwani kuweza kufanya ziara yake katika mji
wa Namugongo nchini Uganda kwa ajili ya ziara ya Kitume.
Akizungumza wakati
wa harambee iliyofanyika katika ukumbi wa TRIPPLE J, Katibu wa kwaya MTAKATIFU
DON BOSCHO, BI.PHILOMENA SHIJA amesema lengo la kuaandaa harambee hiyo ni
kutafuta shilingi milioni 25 kwa ajili ya safari ya Namugongo, Uganda.
BI.SHIJA
ameongeza kuwa mbali ya kutafuta nauli ya kwenda Uganda, harambee hiyo pia
ilikuwa na jukumu la kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa basi ambalo
litawawezesha kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine lenye thamani ya
shilingi milioni 70.
Katibu huyo
wa Kwaya ya MTAKATIFU DON BOSCHO,. Bi.PHILOMENA SHIJA amebainisha kwa hiyo
ambayo ina miaka 30 kutoka kuanzishwa kwake, mpaka sasa imetoa albamu sita.
Naye Mgeni
Rasmi katika hafla hiyo BW.CYPRIAN
MUGEMAZI kwanza aliwapongeza wanakwaya hao kwa kuweza kufanikisha malengo
mbalimbali wanayojiwekea ikiwa na kufanikisha safari yao ya Mkoa wa Kagera.
BW.MUGEMAZI
amewataka wana kwaya hao kuifanya kazi ya uinjilishaji kupitia kwaya ili waweze
kutimiza utume wao kupitia kumuimbia Bwana.
END.
Comments
Post a Comment