MFUKO WA RAIS HOI

MFUKO WA RAIS WA KUJITEGEMEA UMEBAKI JINA TU.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/1/5/2014 10:32:56 AM

Wanachama wa mfuko Rais mjini Kibaha wamelalamikia hatua ya kusumbuliwa na watendaji wa mfuko huo kutokana nakutopewa miko[po wanayohitaji pamoja na kulipa fedha za akiba walizotakiwa kutoa kabla ya kupatiwa mkopo huo.

Mwandishi wa habari hizi akiongea na mmoja wa mmoja wa wanakikundi wa kikundi cha Kiluvya B, Mama EUNICE MACHA ambaye amebainisha kuwa kwa sasa ana takriban miaka isiyopungua sita toka ametoa fedha za akiba kwa ajili ya kupatiwa mkopo huo, lakini imekuwa wakizungushwa mpaka sasa.

Mama.MACHA amebainisha kutokana na hali hiyo biashara zake zimekuwa zikiyumba na kumsababishia maisha magumu na yasiyo na uhakika na akiwa hajui kama fedha zake zikirudishwa zitakuwa na riba au la.

Mama.MACHA ameongeza kuwa amekuwa mteja wa mfuko huo wa Rais kwa kipindi cha miaka 5, na wameanza kudai amana zao toka mwaka 2008, lakini hakuna kilichofanyika kuhusiana na malipo ya akiba za wanachama baada ya mfuko huo wa Rais kushindwa kutimiza majukumu yake.

Naye BI.SARAH KIMARO yeye akiwa mmoja wa  wanachama wa mfuko huo, amekuwa na wakati mgumu kuendesha maisha yake kutokana na kuwa fedha zote alizokuwa anategemea zimeshikiliwa na mfuko huo.

Naye BW.CHRISANT MVULA ameshangazwa na majanga yaliyoiukuta mfuko wa Rais wa kujitegemea uliokuwa na dhima ya kuwasaidia wanachama wake kwa kuwapatia mikopo kwa ajili ya kujikwamua na hali ngumu ya uchumi.

BW,MVULA amebainisha kuwa kabla ya kuingia madarakani serikali ya awamu ya nne mfuko huo ulikuwa ukifanya shughuli zake kwa weledi wa hali ya juu na kuweza kuwasaidia kinamama katika masuala mbalimbali, lakini mara baada ya uongozi wa awamu ya nne kuwa madarakani mfuko huo umekuwa ukipora wananchi wake badala ya kuwasaidia.

Naye Meneja wa mfuko wa Rais wa kujitegemea mjini Kibaha ambaye alikataa kutaja jina lake amethibitisha kupokea malalamiko ya wanakikundi wa Kiluvya B, na amewataka kufika ofisini kwake siku ya Januari 06 mwaka huu, ilikupeana ufafanuzi.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA