WANANCHI WACHUKUA MAAMUZI MAGUMU

WAKOKOTA MAGARI WA JIJI WASHAMBULIWA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/11/13/2013 12:41:27 PM
Hali ya uwepo wa vurugu za mara kwa mara im eanza kuota mizizi kufuatia uwepo kwa sheria ndogo ambazo zinaleta utata mkubwa wa wananchi, kiasi cha kusababisha wananchi kuamua kuchukua hatua mikononi katika suala zima la kutetea na kulinda haki zao.

Leo mwandishi wa habari hizi ameshuhudia kushambuliwa kwa mfanyakazi mmoja wa gari la kukokota magari, mara baada ya mtu huyo ambaye jina lake halikupatikana kufunga mnyonyoro gari la Mam,a mmoja ambaye alipaki gari lake mbele ya soko ili kwenda kupata mahitaji ya nyumbani.

Ndipo gari hiyo maarufu kama BREAKDOWN liliposegea karibu na gari lilokuwa limeegeshwa mbele ya soko na mmoja wa watumishi wa kampuni hiyo alitoa mnyonyoro na kulifnga gari hiyo kitu ambacho wananchi walioshuhudia tukio hilo hawakukubaliana nacho na kuanza kuwashambulia wahusika.

Katika harakati za kutuliza hali ya mambo, Diwani wa Kata ya Mailimoja, BW. ANDREW LUGANO amewataka wananchi kuwa watulivu na kuacha vitendo vyote vya uvinjifu wa amani na hivyo kumpatia nafasi yeye kushughulikia suala hilo.

Diwani huyo wa Kata ya Mailimoja, BW.LUGANO amewaahidi wananchi kwenda kumuona mkurugenzi wa halmashauri ili kupata mwafaka wa suala hilo,ikiwa pamoja na kujenga maegesho ambayo yatakuwa yanatambuliwa rasmi kisheria badala ya kufanya kama wanavyofanya sasa.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA