MASAHIHISHO WAFUGAJI WAILILIA SERIKALI
WAFUGAJI WAILILIA SERIKALI
Ben Komba/PWANI-TANZANIA/11/7/2013 9:33:09 AM
Wafugaji nchini wamemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.JAKAYA KIKWETE Awabebeshe dhamana viongozi wa mkoa Morogoro juu ya watu waliokufa kufuatia mapigano kati ya ushirika unaosimamia masuala ya maliasili na uhifadhi wa misitu ya MWANU na wafugaji.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa wafugaji Tanzania BW.GEORGE KIFUKO amesema tatizo hilo linasababishwa na viongozi wa mkoa wa Morogoro kutokana na uanzishaji wa kamati ambayo inatekeleza operesheni ya kukamata mifugo.
BW. KIFUKO amesema kuwa Mkuu wa wilaya ya Mvomero ndio ameanzisha zoezi hilo kwa maslahi binafsi kwa kukamata ng’ombe na kuwalazimisha wafugaji kulipa shilingo milioni 10 ili kuweza kukomboa ng’ombe hao takriban 300, Jambo ambalo wafugaji hawajakubaliana nalo na kutaka waende mahakamani kwa hatua zaidi jambo ambalo wakamataji hao wa mifugo walikataa.
Amemtaka Rais KIKWETE afikie hatua achukue maamuzi ya kuzuia unyang’anyi wa mali za wananchi, mauaji na kila aina uvunjaji wa katiba ya wananchi na hasa kwa kuzingatia hakua ambaye yupo juu ya sheria.
Naye mfugaji BW.SIMON FAHAMUHERI ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kambala Kata ya Mbiki wilayani Mvomero amemwambia mwandishi wa habari hizi kuwa juzi watu wa MWANU walikwenda kukamata ng’ombe katika eneo la mfugaji na huku wakiwalazimisha wafugaji watoe kiasi cha shilingi Milioni 10.
END.

Comments
Post a Comment